fbpx
apps, Gemu

Gemu ya Pokemon Go yafanyiwa maboresho ya aina yake

gemu-ya-pokemon-go-yafanyiwa-maboresho
Sambaza

Kwa wale wapenzi wa gemu hasa gemu ya Pokemon Go hii ni habari njema ukizingatia gemu hii iliwahi kumhusisha aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Democrats Bi. Hillary Clinton.

Wakati gemu hili linaingia sokoni lilitokea kupendwa sana na kuongeza soko la Nintendo mara mbili zaidi kwa kiasi cha dola za Kimarekani 43 milioni ( zaidi ya Tsh. 94.2 bn) imefanyiwa masasisho ili kuiwezesha kuwa bora zaidi.

INAYOHUSIANA  WhatsApp haina chanzo cha kuingiza Pesa mpaka sasa #Uchambuzi
pokemon
Zaidi ya Pokemon 80 kuwepo kakika gemu hiyo.

Masasisho yaliyomo ndani yake;

  • Maboresho yamefanywa kwenye kuipengele cha “Evolution“. Ieleweke kwamba mwanzilishi/muudandaji  anayejulikana kama Pokemon anatokea maeneo ya Kanto na katika siku za usoni gemu hiyo itahusisha mambo kutoka Johto.
  • Kipengele cha “Berry“. Katika kingele cha berry hapo awali Pokemon ilikuwa ni rahisi kumkamata lakini kwa masasisho ya hivi karibuni haitakuwa rahisi kumkamata kama ilivyokuwa hapo awali.
  • Vitu vipya katika kipengele cha “Avatar“. Hii inajumuisha fulana, kofia na suruali mpya ambayo ni masasisho yanayopatikana katika gemu hili.
INAYOHUSIANA  Flynx: Okoa Muda na Kivinjari Kinachoelea! #Apps

Bado haijawekwa wazi tarehe ambayo masasisho hayo yatapatikana ila kinachojulikana ni kwamba maboresho hayo yatapatikana hivi karibuni.

Je, wewe ni unalipenda gemu hili? Tuambie umeipokeaje habari hii kama mpenzi wa kucheza magemu?

Vyanzo: Fortune, mitandao mbalimbali.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|