Mradi wa kuunda gari lenye kasi zaidi duniani umefufuliwa na tayari gari hilo limeshavunja rekodi ya kwenda maili moja ndani ya sekunde 3.6 🙄 🙄 🙄 .
Mpango wa kuunda gari hilo lililopewa jina ‘Bloodhound’ ulikwama miezi ya karibuni kutokana na matatizo ya kifedha lakini mfadhili mpya amepatikana na tayari limeshaweka rekodi likiangazia kuweka rekodi nyingine mwaka huu.
Wahandisi wakiwa katika harakati za uundaji wa gari linalotegemewa kuwa na kasi zaidi.
Mwezi Oktoba 2017 ni historia ya miaka 20 tangu kuwekwa kwa rekodi ya sasa ya kasi ya gari ardhini ambayo ni Kilomita 1,228 kwa saa (763mph). Rekodi hiyo iliwekwa na gari lililopewa jina “Thrust SSC” jangwani Nevada-Marekani.
The Thrust: Gari lililiowahi kushikillia rekodi ya kuwa na kasi zaidi duniani.
Katika maajribio yatakayofanyika majira ya joto mwaka huu wa 2018 linaangazia kwenda umbali wa 1000mph.
Bloodhound inakadiriwa kuwa na urefu wa mita 13.7 na uzito wa tani 7.5.
Gari hilo linaundiwa Uingereza na liliwasilishwa kwenye maonyesho Canary Wharf, London likiwa bado halijakamilika mwezi Septemba mwaka jana na tangu wakati huo limekuwa Bristol likiwa halifanyiwi kazi yoyote.
Gari hilo litatumia injini ya ndege aina ya injini ya Rolls-Royce Ej200 jet fighter pamoja na roketi kadhaa zilizoiwezesha kwenda umbali wa maili moja ndani ya 3.6.
Katika majaribio yaliyofanyika mwezi Oktoba 2017 Bloodhound ilifanikiwa kwenda umbali wa 200mph ikitafsiriwa kama kasi ndogo ukilinganisha na uwezo wake.
Je, uadhani gari hiyo italeta upinzani kwa magari yenye kasi zaidi kwa sasa? Tupe maoni yako. Â TeknoKona itazidi kukujuza mapya kuhusu gari hili linalosadikiwa kuwa na kasi zaidi kuliko magari yote duniani.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|