fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Galaxy Fold 2: Fununu kuhusu toleo la pili la inayojikunja

Galaxy Fold 2: Fununu kuhusu toleo la pili la inayojikunja

Spread the love

Mwanzoni mwaka jana (2019) dunia ilipata kufahamu uzinduzi wa Samsung Galaxy Fold ambayo kimsingi ilirudisha simu zinazojikunja katika ulimwengu lakini katika sura ya kitofauti kabisa na teknolojia ya kisasa. Mwezi Agosti mwaka huohuo ikaingia sokoni kuanza kuuzwa.

Wakati bei ya mtangulizi wake ikionekana kushuka polepole tayari watu wameshaanza kuona muonekano wa Galaxy Fold 2 ikimaanisha hilo ndio itakuwa toleo la pili kwa simu janja kutoka familia hiyo. Ingawa fununu za rununu husika bado hazijjaanza kufahamika lakini maboresho yanaonekana kwenye muundo, mpangilio wa kamera kama picha ifuatayo inavyojieleza:-

Galaxy Fold 2

Fununu kuhusu muonekano wa Samsung Galaxy Fold 2.

Vilevile, kitu ambacho kimetokea kuwavutia wengi ni kitendo cha ule uwazi wa kuonyesha simu ni ya kukunja/kukunjua mara inapofungwa kutumika kama rununu na si tabiti. Sifa lukuki bado hazijaanza kufahamika lakini siku za usoni tutaweza kufahamu mengi kwani hii ni moja ya simu ambayo inawakumbusha watu miaka mingi nyma wakati teknolojia hiyo ilipoingia mara ya kwanza machoni pa watu.

Galaxy Fold 2

Samsung waamua kuitangaza Galaxy Fold toleo la pili kinamnanamna.

Jinsi ambavyo muundo wa kamera zilivyopangiliwa ni kama kwenye Samsung Galaxy S20+ ingawa hizi ni fununu tu pengine baada ya kutoka ikawa ni ya kitofauti kabisa au ikafanana na hiki ambacho wengine wameanza kukiona.

Vyanzo: Pocket Lint, GSMArena

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania