Shirika lisilo la kifaidi la Mozilla, ambao ni wamiliki wa kivinjari cha Firefox, wamekuja na huduma ya kutuma mafaili ya hadi ukubwa wa GB 1 ambayo hujifuta yenyewe baada ya muda.
Huduma hiyo waliyoipa jina la Firefox Send ipo wazi kwa watumiaji wa vivinjari vya aina yeyote, yaani ata kama ni Chrome au Opera.

- Utaweza kuupload na kutuma file kwa mtu kwa kuweka barua pepe yake baada ya kuupload faili lako kwenye tovuti hii
- Atakayepokea atatumia link kwenye barua pepe yake na atatakiwa kubofya na kushusha/download file hilo ndani ya masaa 24 tokea kutumwa kwake au baada tuu ya kuwa lime’downloadiwa’.
- Baada ya masaa 24 au aliyetumiwa kudownload, mafaili hayo yatajivuta na hayatapatikana tena
- Mafaili yote yanayotumwa kwenye mfumo huo yanapewa usalama wa hali ya juu kupitia mfumo wa ‘encryption’
Kwa sasa huduma hii ipo katika majaribio na maboresho ya mwisho mwisho ila inapatikana kwa mtu yeyote. Utaweza kutuma mafaili ya hadi ukubwa wa GB 1 – labda huko mbeleni uwezo wa kutuma zaidi ya hapo utakuwa wa kulipiwa.