fbpx
Android, Android Go, apps, Google

Files ya Google yaboreshwa usalama wake

files-ya-google-yaboreshwa-usalama-wake
Sambaza

Katika dunia ya leo suala la ulinzi katika ulimwengu wa utandawazi ni kitu ambacho makampuni ambayo yanajishughulisha na teknolojia yamekuwa yakijidhatiti siku baada ya siku na safari hii “Files ya Google” imeongezwa ubora.

Sote tunatumia vifaa vya Android toleo la kisasa ama wale ambao tunatumia Android Go tunafahamu vyema kuwa kuna programu tumishi iitwayo Files ndani ya rununu zetu mahususi kwa ajili ya kutunza vitu (picha, nyaraka, picha mnato, n.k) ambapo mtumiaji anaweza akafungua vitu alivyovihifadhi humo wakati wowote hata bila ya kutumia intaneti.

Mwaka 2017, “Files” ilionekana kwa mara ya kwanza kwenye toleo la Android Go huku ikilenga kumsaidia mtumiaji kuweza kupunguza vitu kwenye simu janja kiurahisi hivyo kufanya rununu kuwa na memori kwa matumizi mengineyo.

FIles ya Google
Tangu kuanzishwa kwake Google wameshafuta vitu zaidi ya trilioni 1 lakini pia kuokoa PB 400+ ya memori kutoka kwenye simu za watu.

Sasa katika maboresho “Files ya Google” imeongezwa ulinzi wa kuweka faili waliloliita “Safe folder” ama faili salama (kwa mujibu wa tafsiri isiyo rasmi) ambapo mtumiaji ataweza kuweka ulinzi kwa kutumia nywila/nenosiri na itahitajika kila mara ambapo mtu atataka kukuona vilivyowekwa huko.

INAYOHUSIANA  iCloud kuhamia China, Je itakuwa kwa kila mtumiaji? Fahamu zaidi

Pili, kwa chochote ambacho kitawekwa huko basi kitatoweka ile sehemu ambayo ilikuwa ikionekana hapo awali kulingana na aina ya kitu husika. Iwapo mtu mtu atataka kuona vitu vilivyofichwa atalazimika kuweka nywila kuweza kujua kilichomo ndani ya “Safe folder“.

Files ya Google
Ulinzi wa kutumia nenosiri ndani ya faili salama kwenye Files.

Maboresho hayo kwa sasa yapo katika hatua ya majaribio ingawa yatapatikana katika siku za usoni. Tuambie mtazamo wako kuhusiana na hili ewe msomaji wetu unayependa usalama/faragha ya vitu vyako.

Vyanzo: Gadgets 360, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|