fbpx
Ndege, Tanzania

FastJet kupata ndege mpya, Embraer E190. Ifahamu Zaidi

fastjet-kupata-ndege-embraer-e190
Sambaza

Kampuni ya usafiri wa ndege maarufu nchini ya FastJet ipo njiani kutambulisha ndege yao mpya, ndege hiyo ni Embraer E190.

Kampuni ya ndege ya Embraer ni ya nchini Brazili inayojihusisha na utengenezaji wa ndege za abiria, za kijeshi, kilimo na ata za kutumiwa na makampuni binafsi (mabosi).

Kampuni ya ndege ya FastJet Embraer E190
Ndege ya Embraer E190
Eneo la kuendeshea ndege

Ndege ya Embraer E190 ni toleo lao la ndege la abiria kutoka familia ya ndege za E-Jet kutoka kampuni ya Embraer. Ndege za Embraer E190 zimetengenezwa kubeba kati ya abiria 96 hadi 114 kulingana na chaguo la aina ya viti kutoka kwa kampuni nunuaji.

Ndege ya kwanza ya E190 ilirushwa Februari 19 mwaka 2002, ila kuanzia Machi 2004 ndio ndege ya kwanza ya Embraer E190 ilipokewa na mteja wa kwanza, ambapo ilikuwa ni kampuni ya ndege ya LOT Polish Airlines, ya nchini Polandi.

Brazil ni moja ya mataifa machache yaliyofanikiwa kuwa na kampuni kubwa ya utengenezaji ndege duniani.

Ndege hii inauwezo wa kubeba hadi kilogramu 13,047 ya uzito (abiria na mizigo), na ikaweza kuruka hadi umbali wa km 4,537 kutoka usawa wa bahari.

INAYOHUSIANA  C919: China bado wapo nyuma katika kuleta ndege yao ya kwanza ya abiria

Vyanzo vinaonesha bei ya ndege hiyo ni kati ya dola za Marekani milioni 46.2 (Takribani Tsh Bilioni 103).

FastJet inategemea kuanza kuitumia katika baadhi ya safari zake kuanzia katikati ya Novemba mwaka huu.

Vyanzo: Corporate-digest.com, Embraer na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |