Faragha ama usiri ni kitu muhimu kwa kila mtu na makampuni mengi duniani yanajitahidi kuboresha teknolojia na kulinda data za wateja wao. Suala la kuweka usiri kwenye jumbe za watu imekuwa ni kitu ambacho makampuni kama Google, Facebook na wengineo wakitekeleza kwa vitendo.
Kwa wale wote ambao tunatumia simu janja za Android kwa hakika tunafamu Google Messages; programu tumishi ambayo inawezesha kutuma/kupokea ujumbe mfupi wa maanshi na hata picha ama picha mnato. Kwa muda mrefu tuu Google walikuwa hawajapeleka teknolojia ya usiri kwenye programu hiyo tumishi lakini hilo sasa limefikia tamati!
Jumbe tuzotuma kwenda kwa mtu mmoja hadi mwingine kwamba anayweweza kuona ni wewe na yule anayepokea tu hapo awali ilikuwa ndani ya Google Messages toleo la Majaribio lakini sasa inapatikana kwa watu wote wenye simu simu za Android.

Teknolojia hii ina maana ya kwamba hakuna ambae ana uwezo wa kusoma jumbe zako kwani unakuwa umefungwa katika mtindo wa sifuri na moja (lugha ya kompyuta) na mara baada ya kufika kwa mhusika simu inaubadilisha na kuuweka katika maandishi ambayo yanaeleweka.
Teknolojia hii ni sawa tuu na ile ambayo inatumiaka kwenye WhatsApp, Telegram, Facebook Messenger, n.k na sasa ndani ya Google Messages. Kwa hakika hii ni habari njema kwa watu wote ambao tunapenda faragha na data zetu kuwa salama.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.