fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kivinjari Teknolojia

Fanya Kivinjari Cha EDGE Kufuta Taarifa NYETI Za Kimtandao Pale Unapokifunga!

Fanya Kivinjari Cha EDGE Kufuta Taarifa NYETI Za Kimtandao Pale Unapokifunga!

Ni wazi kwamba kuna taarifa zingine za kimtandao ni siri, lakini licha ya hili ni wazi kwamba ni vizuri kwa mtu kufuta taarifa zake mara kwa mara pindi anapomaliza kutumia kompyuta

Taarifa hizi zinaweza zikawa kama ni nywila n.k. vile vile fikiria kwa mfano kama watu wanatumia kompyuta ya aina moja? hapa ndio jambo hili linazidi kuwa la muhimu zaidi kufuta taarifa hizo kila baada ya kutumia kivinjari.

Kama unatumia microsoft edge katika kompyuta yako basi leo TeknoKona inakujuza ujanja huu. Lakini kingine cha kujua ni suala la taarifa ambazo zitaweza futika: nazo ni

  • kumbukumbu ya mitandao uliyopitia (mfano. www.teknolojia.co.tz) kupitia kivinjari
  • kumbukumbu ya vitu ulivyoshusha (download) kupitia kivinjari
  • Taarifa za ‘cookies’ na zingine zingie
  • mafaili au picha ambazo zimejificha katiaka sehemu ambayo ni ngumu kuzipata kwa haraka (cached files & photos)
  • neno siri (password) ambazo ulijaza katika mitandao mbali mbali wakati unatumia kivinjari
  • taarifa ambazo huwa zinajijaza mara kwa mara (autofill form data)
  • ruhusa za kimtandao  (site permission)

Hapo awali ilikua kama unataka kufuta yote haya basi ulikua huna budi kwenda kufuta katika eneo la settings pindi tuu ukimaliza kutumia kivinjari. lakini vipi kama utaweza kufanya hivi wakati unamaliza tuu kutumia kivinjari chako cha edge?

Eneo La Vidoti Vitatu Katika Kivinjari Cha Edge

Eneo La Vidoti Vitatu Katika Kivinjari Cha Edge

Kwa kuanzia kabisa fungua kivinjari chako cha microsoft edge kwa kutumia kompyuta na kisha ingia katika vidoti vitatu kule upande wa juu

Eneo La Settings Katika Kivinjari Cha Edge

Eneo La Settings Katika Kivinjari Cha Edge

Ikishatoka window nyingine hapo ingia katika eneo la settings

SOMA PIA  Njia Mbadala ya Kutumia WhatsApp kwenye Firefox kwa Kuona na Kujibu Ujumbe kwa Haraka

Baada ya hapo ingia katika eneo la “Privacy, Search, and Services” kisha ingia katika eneo la “Clear Browsing Data” na ingia katika chaguo la “Choose What To Clear Every Time You Close The Browser” kisha fanya machaguzi

Maeneo Ya “Privacy, Search, and Services” na “Clear Browsing Data” Katika Kivinjari Cha Edge

Maeneo Ya “Privacy, Search, and Services” na “Clear Browsing Data” Katika Kivinjari Cha Edge

yatatokea machaguo mengi ambayo unaweza kuchagua, kila chaguo ambalo utachagua basi hii inamaanisha kuwa kila ukimaliza kutumia kivinjari cha edge kila unapokifunga basi kitakuwa kinafuta taarifa zote hizo ambazo umezijachua zifutwe.

SOMA PIA  Twitter waleta Chati za Makundi na Uwezo wa Video

Niambia hii umeipokea vipi? je njia hii ulikuwa unaijua? niandike hapo chini sehemu ya maoni, ningependa kusika kutoka kwako.

Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Kivinjari Cha Edge Hapa

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania