Fairphone: Simu janja inayoruhusu ubadilishaji wa vipuli kwa urahisi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu ya Fairphone ni simu janja ambayo ukishainunua haikupi ugumu tena kubadili kitu kama kamera, betri n.k, tena unaweza fanya mwenyewe.

Kampuni iliyopo nchini Uholanzi iliyoanzishwa mwaka 2010 inalenga kutengeneza simu janja ambayo mtumiaji wake ataweza kubadili na kununua vipuri vipya vilivyo bora au kubadilisha vilivyoharibika kwa urahisi.

simu ya fairphone

Simu hiyo inakuja na ‘screwdriver’ ya kukuwezesha kuifungua na kuweza kubadili vitu vingi ndani yake

Ukinunua simu yako utakuta ndani yake kuna vifaa vya kukusaidia kuifungua kwa urahisi na kubadili vitu kama vile kamera, betri, na vingine vingi ambavyo kwenye simu zingine ni vigumu kwa mtu kufanya mabiliko hayo.

INAYOHUSIANA  Ijue Simu mpya ya mkunjo yenye vioo viwili ya Samsung Galaxy W2018

Lengo kuu ni kuhakikisha mtu anaweza kukaa na simu kwa muda mrefu bila ulazima wa kutumia pesa nyingi katika kununua simu mpya ili aweze tuu kupata kamera nzuri zaidi n.k.

Tayari kwa wastani watumiaji wa simu janja siku hizi wanakaa na simu kwa muda mrefu zaidi bila uhitaji wa kubadili simu na kupitia Fairphone lengo ni kufanya jambo liwe la kawaida na lenye manufaa kwa harakati za utunzaji mazingira.

INAYOHUSIANA  TTCL kujenga kiwanda cha utengenezaji simu nchini

fairphone

Kupitia tovuti yao watumiaji wanaweza kununua vipuli/part za simu hiyo kwa urahisi sana.

Sifa ya Fairphone 3 (toleo la sasa) linalouzwa kwa takribani Tsh Milioni 1.1 – 1.2 za kitanzania ni kama zifuatazo (ukishanunua bado una uwezo wa kuongeza uwezo mbalimbali kwa kununua vipuli vipya);

  • Programu endeshaji: Android 9, toleo safi la bila mbwembwe nyingi
  • Prosesa: Qualcomm Snapdragon 632 ikija na RAM ya GB 4
  • Diski Uhifadhi: GB 64 na ukiwa na uwezo wa kuoongeza kupitia eneo la microSD
  • Betri: mAH 3,000
  • Display: Full HD, inchi 5.65
  • Kamera: Megapixel 12, f/1.8, wakati kwa selfi ni Megapixel 8, f/2.0
INAYOHUSIANA  Ujio wa iPhone Mpya-Watu Waweka Kambi Nje ya Maduka!

Teknolojia zingine ni pamoja na uwezo wa 4G, laini mbili, Eneo la ulinzi wa utambuzi wa alama za vidole, na kitundu cha earphone.

Toleo la Fairphone 3 linakuja sokoni hivi karibuni na watu wanaweza kununua simu hiyo moja kwa moja kwenye tovuti yao na wao watatuma popote ulipo.

Je una mtazamo gani juu ya simu ya namna hii?

Chanzo: Tovuti yao – https://shop.fairphone.com/en/
Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.