fbpx

Slack, Teknolojia, Uchambuzi

Fahamu Slack Ni Mtandao Wa Aina Gani?

fahamu-slack-ni-mtandao-wa-aina-gani

Sambaza

Kwenye dunia ya leo teknolojia imerahisisha mambo mengi ambayo hapo awali ilikuwa yalichukua muda mrefu kukamilika kutokana na sababu mbalimbali lakini hivi leo vitu ni tofauti mfano uwepo wa kitu kinachoitwa “Slack“.

Hivi leo unaweza kuwana/upo kwenye taasisi, kampuni, shirika, n.k ambapo pamoja na matumizi ya kompyuta lakini kila mfanyakazi inambidi kuwepo kazini kila siku asubuhi kutekeleza majukumu yake. Vilevile, unaweza ukawa mmliki wa kampuni fulani lakini hauna mfumo ambao unakukutanisha wewe na wafanyakazi wako kuweza kupata mrejesho, kukagua kazi, n.k pasipo kuonana ofsini na ndio hapo “Slack” inaingia.

Slack ni nini?

Huu ni mfumo ambao unaweza kutumiwa na mtu, kampuni (kubwa/ndogo) au taasisi ili kuweza kuwasiliana, kupata mrejesho, kugawa kazi huku kila mmoja akiwa mahali pake (bila ya kukutana ana kwa ana).

Mtu anaweza kutekeleza majukumu yake kwenye Slack kwa kutumia kompyuta au simu ya mkononi lakini bila kusahau uwepo wa intaneti.

Mtandao wa Slack
Mtandao wa Slack unaoweza kukutanisha watu na wakatekeleza majukumu yao, kuwasilisha wakiwa sehemu yoyote ile.

Vitu gani vinaweza kufanyika kwenye Slack?

i) Kutengeneza timu. Wewe kama mmiliki wa kampuni baada ya kuweka mpangilio sawa kwenye Slack kinachofuata ni kuwaalika ambao unataka kufanya nao kazi kwa kuwatumia kiunganishi cha mwaliko ambapo mhusika atabofya na ukurasa utafunguka kisha kujaza taarifa zake ambazitamuwezesha kurudi tena mara baada ya kutoka kwenye mtandao husika.

INAYOHUSIANA  Wiki ya Ubunifu chini ya Shirika la HDIF Yaanza Rasmi! #InnovationTZ

Hapa utaweza watu wa kwenye timu yako katika madaraja tofauti mathalani:

   a) wamiliki (kama utapenda awepo zaidi ya mmoja)-kuandaa sehemu ya kufanyia kazi na kuwaweka watu katika madaraja,

   b) viongozi-wanamsaidia “Mmiliki” kuongoza timu (wafanyakazi),

   c) wanachama/washiriki-wanao uwezo wa kuwasiliana/kutuma kitu kwenda kwa yeyote aliyopo kwenye mfumo wa Slack kupitia kampuni/taasisi fulani,

   d) wageni-hawa wanaweza kuwasiliana/kutuma kitu kwa mtu fulani tu.

INAYOHUSIANA  iPant? Hii Kwa Ajili Ya iPhone 6 Plus!

ii) Mawasiliano/Mazungumzo. Hapa inawezekana kumpigia mtu simu, kutumia/kutafuta ujumbe, kutengeneza chaneli ambayo itawezesha waliwekwa humo tu kuweza kutuma kitu ambacho wote waliomo humo watakiona,

iii) Kununua huduma. Kwa kawaida mtandao wa Slack ni BURE ingawa kuna huduma nyingnine zinakuwa hazipatikani mpaka kwa kulipia kiasi fulani cha pesa. Hivyomtandao wa Slack umegawanyika katika makundi matatu:

   a) standard– kwa ajili ya biashara ndogo/katikati. Hii gharama yake ni $6.67/mwezi|zaidi ya Tsh. 15,000,

INAYOHUSIANA  Makampuni 10 Yanayoongoza Kupata Maombi Ya Kazi Kupitia LinkedIn! #Teknolojia

   b) plus-kwa ajili ya kampuni kubwa au zile zinazotafuta nyenzo za hali ya juu kufanya kazi. Hii gharama yake ni $12.50/mwezi|zaidi ya Tsh. 28,000 na

   c) enterprise grid-kwa kampuni/taasisi kubwa zaidi au zile ambazo zinafanya uangalizi wa karibu zaidi. Kujua bei kwenye kipengele ni mpaka kufanya mawasiliano na idara ya masoko ya Slack.

Mtandao wa Slack
Mtandao wa Slack ukiwa umeshapangiliwa vizuri na tayari washiriki wameshaletwa sehemu moja.

Unajiuliza utaihamishaje ofisi yako iwe na uwezo wa kutekeleza majukumu yake popote pale? BOFYA HAPA ili kuweza kuandaa muudo wa ufanyaji kazi kidijitali.

Chanzo: Slack

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|