fbpx

FAHAMU: Mega Pixel (MP) Ni Nini Na Inafanya Nini Katika Picha!

0

Sambaza

Mmoja kati ya wasomaji wetu ameomba tuandae makala juu ya Mega Pixel (MP). Najua neno hili tunalisikia sana na kuliona katika kamera lakini je, tunajua linamaanisha nini?

Leo TeknoKona Tupo Bega Kwa Bega Kukupa Somo Juu Ya Mega Pixel.

Kwa kabla ya Mega Pixel inabidi kujua Pixel ni nini. Kwa haraka haraka Pixel ni viboksi boksi vidogo vidogo ambayo vinatumiaka katika kuijenga picha mpaka kukamilika (ikaonekana).

Mfano Wa Viboksi (Mega Pixel / Pixel) VInavyotumika Kujenga Picha

Mfano Wa Viboksi VInavyotumika Kujenga Picha

Viboksi boksi (pixel) hivi vikiwa ni vingi zaidi hii inamaanisha kuwa ndio picha yako itakapo kuwa nzuri pia na kinyume chake ni kweli pia.

MegaPixel (MP)  ni mkusanyiko wa Pixel milioni moja,  hapa vile vile uzuri wa picha utaweza kuonekana kwa kuangalia ni Pixel ngapi zimejikusanya katika kujenga picha hiyo.

Siku hizi watengenezaji wa kamera wengi huwa wanatangaza biashara yao ya kamera hasa kwa kusema vifaa vyao viina Mega Pixel (MP) ngapi kama njia moja ya kuwavutia watu na bidhaa hiyo.

Kwa mfano kamera yenye Mega Pixel (MP) 8 kwa haraka haraka itakua na viboksi boksi vidogo vidogo milioni 8 kwa kila inch ambavyo vitatengeneza picha itakayopigwa na kamera hiyo.

La kumalizia ni kwamba tukiwa na viboksi boksi (pixel) vingi hii inamaanisha kuwa picha zetu zitakuwa nzuri. Kumbuka picha ikipiga na kamera yenye Pixel chache ukii’zoom’ utaona kabisa alama za viboksi boksi zikiambatana na ukungu.

Baada Ya Ku'zoom' Picha Utafanikiwa Kuona Baadhi Ya Mega Pixel (Pixel)

Baada Ya Ku’zoom’ Picha Utafanikiwa Kuona Baadhi Ya ‘Pixel’

Laikini Mega Pixel zikiwa ni za kutosha utaweza hata kui’crop’ picha hiyo kwa urahisi na bado ikawa inaonekana ni nzuri tuu.

Niandikie hapo chini sehemu ya comment, hii umeipokeaje? ningependa kusikia kutoka kwako.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.