fbpx

Apple, IPhone, Kamera, Teknolojia

FAHAMU Teknolojia Ya LiDAR Kwenye Baadhi Ya iPhone!

fahamu-lidar-kwenye-iphone

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Tangia iPhone 12 Pro ilivyotoka ndio simu ya kwanza kutoka Apple ambayo imekuja na teknolojia ya LiDAR, tumeona vipengele vingi vipya kuja na hii ikiwa ni kama sehemu ya Apple kuboresha zaidi simu zao.

Kwa ulimwengu wa simu ilikua ni kitu kipya, na maswali yamekuwa ni mengi sana juu ya teknolojia hiyo na ufanyaji wake wa kazi. Kirefu cha LiDAR ni ‘Light Detection and Ranging’,

Sensa Ya LiDAR iPhone
Sensa Ya LiDAR iPhone

Teknolojia ya LiDAR ipo toka zamani japokuwa katika simu imekuja¬†juzi juzi tuu! Kwa haraka haraka teknolojia hii inafanya kazi hivi; ni kwamba sensa inatoa miale (kama ile ya ‘infrared)¬† mpaka kwenye kitu/umbo alafu miale hiyo inarudi katika sensa ikiwa na taarifa kamili za kitu/umbo hilo (mfano, ukubwa na upana).

LiDAR inapatikana katika kamera za iPhone 12 Pro, pengine itaendelea kupatikana katika simu zingine ambazo zitatokaa kama matoleo ya mbele kwa iPhone 12.

Teknolojia hii katika iPhone 12 Pro haina utofauti sana wa ufanyaji kazi maana ipo kama teknolojia ile ya ‘Face ID’ tofauti kubwa inakuwa ni umbali tuu ndio unatofautiana, kwa ‘Face ID’ inafanya kazi sura ikiwa karibu zaidi.

Mfano Wa Ufanyaji Kazi Wa LiDAR Ndani Ya iPad
Mfano Wa Ufanyaji Kazi Wa LiDAR Ndani Ya iPad

Kingine kizuri kutokana na LiDAR ni kwamba picha za mfumo wa ‘Portrait’ zinakuwa na uhalisia zaidi ukilinganisha na iPhone ambazo hazina teknolojia hiyo kama vile iPhone 11 na matoleo mingine ya nyuma.

SOMA PIA  Mauzo ya Kamera yazidi kuporomoka, sababu ni mauzo ya simu janja

Teknolojia hii inatumika kwa kisai kikubwa katika magari yanayojiendesha yenyewe. Ukiachana na magari, kwa sababu teknolojia hii inaboresha sana eneo la kamera ya simu kuna vitu vingi sana vimebadilika hata App ambazo zinahitaji matumizi ya kamera ili zifanye kazi zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Ufanisi Wa LiDAR Katika App Ya Measure
Ufanisi Wa LiDAR Katika App Ya Measure

Fikiria kama App ya vipimo (measure) katika iPhone itaweza kutoa vipimo sahihi kulinganisha na matoleo ya nyuma ya simu ambazo hazina teknolojia hii.

SOMA PIA  Programu wezeshaji inayoweza kujua unachofikiria

Kuna michezo (games) ambayo kwa kiasi kikubwa inatumia kamera kwa mfano kama Pokemon Go kwa kutumia kamera ambayo ina teknolojia hii ya LiDAR utaweza kulifahidi zaidi.

Kwa sasa teknolojia hii inapatikana katika iPhone 12 Pro (zote) na iPad Pro tuu

Niambie hapo chini katika boksi la maoni, hii umeipokeaje? je unahisi ni teknolojia sahihi kuwepo katika kamera ya simu kwa kipindi hichi?

Tembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: , ,

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*