fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Fahamu kuhusu Spyware
Spread the love

Spyware” ni programu ya kupeleleza iliyotengenezwa kwa nia ya kuingizwa kwenye kompyuta yako, kukusanya taarifa zako na kuzisambaza kwa mtu mwingine. Kifaa chako cha kielektroniki kinapoingiliwa na Spyware huathiri utendaji kazi wake wa kupata mtandao na hivyo kupunguza kasi ya shughuli zako.

Kuna njia mbalimbali ambazo kompyuta yako au simu juanja yako inaweza kuingiliwa na spyware ikiwemo kupakua programu mtandaoni, kuperuzi kwenye tovuti zisizo salama na kupitia viambatanishi vilivyo ndani ya mafaili au kwenye ujumbe wa baruapepe. Spyware inapoingia kwenye kifaa chako inachunguza, kunasa na kutuma taarifa za mambo mbalimbali unayoyafanya kwenye kifaa chako kama vitufe unavyobofya na mitandao unayotembelea.

SOMA PIA  Xiaomi wawatania Apple kwa kuuza bidhaa kwa mafungu kwa majina ya XR, XS na XS Max

Madhara mbalimbali unayoweza kupata kwenye kompyuta au simu janja yako inapoingiliwa na Spyware ni pamoja na kuibiwa taarifa zako binafsi, kuibiwa utambulisho wako mtandaoni na hii hutokea pale ambapo mvamizi ataamua kutumia akaunti zako za mtandaoni pamoja na zile za mitandao ya kijamii. Spyware pia inaweza kukuharibia kompyuta yako kwa kuichosha na kazi mbalimbali ambazo hufanyika hata mmiliki asipokuwa anaitumia kompyuta yake.Fahamu kuhusu spyware

SOMA PIA  Fahamu Skendo Kubwa ya Kampuni ya Magari ya Volkswagen Inayohusisha Kudanganya Kwa Kutumia Teknolojia

Unajuaje kama simu au kompyuta yako imeingiliwa na Spyware?

Baadhi ya dalili za kifaa chako kuingiliwa na spyware ni pamoja na kifaa chako kuwa kizito kufanya kazi au kuharibika ghafla, kujaa kwa nafasi ndani ya kifaa chako bila sababu ya msingi na kutumiwa matangazo mbalimbali ya mtandaoni ukiwa mtandaoni na hata usipokuwa mtandaoni.

Tahadhari za kuchukua kujiepusha na Spyware ni pamoja na:

  1. Kutoingia kwenye tovuti unazotumiwa kwa njia ya ujumbe mfupi au barua pepe zisizoaminika.
  2. Kupakua programu kwenye tovuti zake maalum kama Appstore na Playstore.
  3. Kupakua programu yziada kwa ajili ya kulinda kompyuta yako na kuchunguza matumizi yako ya mtandao.
SOMA PIA  Airtel Care - App inayorahisisha huduma mbalimbali kwa wateja wa Airtel

Mwisho kabisa Spyware inaweza kukuletea kero unapotumia mtandao kwa kukutumia matangazo mbalimbali, kukupeleka kwenye tovuti usizotarajia na pia kuipunguzia kasi kompyuta yako.

Soma zaidi kuhusu Spyware hapa. Endelea kutembelea tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake. Soma makala zetu nyingine hapa.

Chanzo: Kaspersky

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania