fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Magari Teknolojia Tesla Uchambuzi

Fahamu kuhusu Magari ya Umeme na Sifa zake

Fahamu kuhusu Magari ya Umeme na Sifa zake
Spread the love

Magari ya umeme ni magari yanayotumia mota moja au zaidi ya umeme inayotoa nishati kwenye betri. Ubora wa betri ya magari haya hutofautiana na aina ya gari lakini kwa upande wa sifa za jumla yote hayatoi moshi na wala hayana kelele wakati yanatembea.

Kuna kampuni chache mpaka sasa zinazotengeneza magari haya ikiwemo kampuni ya Tesla, Audi, Volkswagen na Hyundai. Baadhi ya magari ya umeme yaliyotengenezwa na kampuni hizi pamoja na zingine ni:

SOMA PIA  Ulemavu wa macho na matumizi ya simu janja

Tesla Model Y: Gari hii inatengenezwa na kampuni ya Tesla na kwa upande wa magari ya umeme hii ndio gari inayoongoza kwa mauzo. Mpaka sasa zimenunuliwa takriban gari 132,000. Gari ya Tesla Model Y ina uwezo wa kutembea mpaka kilomita 524 bila kuchaji upya.

Magari ya umeme

Picha: Muonekano wa Gari ya Tesla Model Y

Audi e-tron: E-Tron ni toleo jipya la gari la umeme lililotengenezwa na kampuni ya Audi iliyopo nchini marekani. Gari hili linasifika kwa vitu vingi mbali na kutumia umeme, linachaji haraka na pia lina uwezo wa kutunza chaji ya kusafiria kilomita 254. Mpaka sasa yamenunuliwa magari zaidi ya 7790.

Magari ya umeme

Picha: Muonekano wa Gari ya Audi e-tron

Porche Taycan: Porche ni kampuni kubwa ya utengenezaji wa magari na hivi karibuni imetengeneza pia na yenyewe gari ya umeme toleo la Porche Taycan. Gari hii ina spidi hadi kufikia kilomita 260 kwa lisaa (260km/hr) na lina uwezo wa kutunza chaji ya kusafiria kilomita 265. Mpaka sasa kampuni ya porche imeuza magari 7228 ya aina hii.

Picha: Muonekano wa Porche Taycan

Volkswagen ID.4: Volkswagen ni kampuni ya kijerumani ya utengenezaji wa magari. Kampuni hii imekuwa ikitengeneza magari mazuri na imara kwa zaidi ya miaka 60 sasa. Volkswagen ID.4 ni toleo jipya la gari za Volkswagen linalotumia umeme. Gari hii inatunza chaji inayoweza kuifikisha hadi kilomita 402 bila kuchajiwa upya. Zimeshanunuliwa gari 12280 mpaka sasa.

Magari ya umeme

Picha: Muonekano wa Gari ya Volkswagen ID 4

Endelea kutembelea tovuti yetu kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania