Tulishaandika kuhusu mipango ya mtandao wa Facebook kuleta Emoji mpya ili kuzidi kuongeza vionjo nje ya kitufe cha ‘LIKE’ kilichokuwepo kwa muda mrefu. Emoji hizo zaanza kupatikana.
Emoji hizi zitasaidia watu kuweza kuonesha hisia zao bila ulazima wa kuandika. Ingawa hichi sio kitu kilichoitajika zaidi na watumiaji wengi lakini kimewafurahisha wengi.
Watumiaji wengi wamekuwa wanataka kitufe (button) cha UNLIKE kama alama ya kuonesha hawajapendezwa na kile kinachowekwa na mtu mwingine (status, picha n.k) lakini mtandao huo unaepuka kuweka kitu hicho.
Facebook Reactions: Emoji mpya

Emoji zilizoletwa zinasaidia kuonesha; Uzuni, Tabasamu, Mshangao, Kicheko, Mapenzi(Kupenda) pamoja na cha Hasira.
Tayari emoji hizo zimeaanza kuonekana kwa watumiaji mbalimbali, kama bado kwako hazijatokea basi subiri kidogo na muda wowote zitaanza kuonekana.
Je, una maoni gani juu ya Emoji hizi mpya? Tuambie kupitia eneo la ‘Comment’.
One Comment
Comments are closed.
[…] Soma: Facebook reaction; Sasa facebooksa zaidi ya like, waleta emoji. […]