fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Intaneti

Facebook kuwapa watumiaji uwezo zaidi wa kile wanachokiona wakiingia. #Timeline

Facebook kuwapa watumiaji uwezo zaidi wa kile wanachokiona wakiingia. #Timeline

Facebook kuwapa watumiaji uwezo wa kuchagua zaidi kile ambacho kinatokea eneo la nyumbani la huduma hiyo, yaani Timeline. Sehemu inayokupa taarifa ya yanayojiri kutoka kwa marafiki, makundi na kurusa unazofuatilia.

Uamuzi huu unakuja ili kusaidia dhidi ya shutuma za muda mrefu za jinsi mfumo wa kikompyuta (algorithm) umekuwa ukichagua vitu vya kutokea na kutokutokea katika eneo la Timeline la mtumiaji wa app hiyo.

Facebook kuwapa watumiaji uwezo

Facebook kuwapa watumiaji uwezo mkubwa wa masuala yanayotokea kwenye timeline

 

SOMA PIA  Engage: App maalum kutoka Twitter kwa ajili ya mastaa

Je, nini kipya kinakuja?

Wanaleta uwezo wa kuchagua aina gani ya mpangilio wa eneo hilo unataka kuangalia. Kutakuwa na;

  • Lililopo kwa sasa, mpangilio unaochaguliwa na mifumo ya kimpyuta ya Facebook, algorithm.
  • Kihistoria, yaani utaweza kuona habari mpya zaidi juu kutoka kwa marafiki, kurasa unazofuatilia na mazungumzo ya makundi (Groups).
  • Kutoka kwa kundi lako binafsi – hapa utaweza kuchagua kurasa, makundi na watu wako wa muhimu ambao hutaki kukosa habari zao.
SOMA PIA  Microsoft Office 2021 inakuja kwa Windows na MacOS mwaka huu

Facebook wamesema uwezo huo wa kuchagua utakuwa kwa watumiaji wote. Kingine kipya kinacholetwa ni pamoja na kuwapa watu uwezo wa kuchagua nani wa kuwaruhusu kuacha maoni yao kwenye machapisho (post) zao. Hivyo utaweza kuamua kama ni wale uliowaowataja kwenye chapisho tu ndio wataweza kutoa maoni yao, au marafiki au mtu yeyote kwenye tovuti hiyo.

SOMA PIA  Facebook kuwasaidia wasioona kuweza kuona picha! #Teknolojia

Vipi una mtazamo gani na maboresho haya kutoka kwa Facebook?  Tuambie kwenye sehemu ya kutoa maoni, usisahau kusambaza kwa wengine.

Vyanzo: Facebook News
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania