Mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook nambari moja kwa umaarufu na kuwa na watumiji wengi sana kila leo imekuwa ikijaribu kujidhatiti katika huduma yao wanayoitoa kila siku.
Matukio ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitokea kila mara kwa kiasi fulani Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuzuia machapisho ya aina fulani ambayo yalikuwa kama kichochezi kufanikisha jambo fulani.
Mtandao wa kijamii wa Facebook umetoa tamko kwamba unataka kujitenga na mazingira ya uhasama kwa watu wanaoweka maudhui tata au watu wenye viashiria/matendo ya kigaidi.
Kauli hii kutoka Facebook imekuja baada ya matukio ya kigaidi ambayo yaliikumba Uingereza zaidi ya mara moja! na waziri mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May kuzitaka kampuni zinazojihusisha na masuala ya teknolojia kuchukua juhudi za makusudi kukabiliana na maudhui yenye mrengo wa kigaidi.
Ni wazi kwamba makampuni makubwa ya kimtandao zisipokuwa makini zitakuwa zinatoa nafasi kwa vikundi vya wanamgambo wenye itikadi kali kuzaliana. Facebook imetamka kwamba kuanzia sasa itakuwa ikiondoa mara moja, maudhui yenye viashiria vya ugaidi.
Soma pia: Matatani kwa sababu ya kubofya “Like” kwenye Facebook
Mtandao wa Twitter wao wamejinasibu kwamba kazi hiyo yakuondoa ama kufutilia mbali maudhui tatanishi na kamba mwaka wa jana pekee ulifanikiwa kuondoa maudhui ya aina hiyo kutoka katika akaunti elfu nne.
Chanzo: BBC
One Comment
Comments are closed.