Kama ilivyo katika App ya Snapchat, ukiifungua tuu unaweza ukaanza kuchukua video au kupiga picha (hata katika mfumo wa selfie). Kutokana na mfumo huu wa kamera, Facebook nao wako mbioni kuuleta kwa watumiaji wao.
Kumbuka mfumo huu una mambo mengi ukiachana na kupiga picha/video, baada ya kupiga picha au kuchukua video unaweza ukaongezea mbwembwe katika kazi zako hizo.
Kingine ni kwamba baada ya Instagram (ambayo inamilikiwa na Facebook) kuanzisha mfumo wa ‘stories’ ambao inasemekana waliuiga kutoka Snapchat, sasa Facebook na yenyewe imeona iige mfumo wa kamera kama ule wa Snapchat.
Lakini kwa mtazamo wangu hii ni nzuri pia. Kumbuka kuna mazingira mengine ambayo unaweza kuwa ikawa ni vigumu kwako kuandika status. Fikiria kama huwezi kuandika ‘status’ hiyo si unaweza tuu ukarekodi/ukajirekodi kavideo Fulani hivi ukielezea hali iliyopo?
Kwa sasa huduma hii inajaribiwa huko nchini Brazil na Canada, pia inakuja na mbwembwe mbwembwe (Filters) nyingi zikihusisha mashindano ya Olympics. Mambo yakijipa na sisi wa huku tutaanza kuifurahia huduma hii pia.
Hii inaonekana kwamba moja kati ya malengo makubwa kwa Facebook ni kwamba sasa inataka kujikita sana katika Video, angalia Snapchat ilivyojipatia umaarufu mkubwa kupitia video. Hata Instagram na Facebook baada ya kuanzisha mfumo mzima wa kuweza kutuma video wamejipatia faida nyingi sana.
Angalia Video Hii Uweze Kujionea Kwa Undani Mambo Ambayo Yanaweza Fanyika Kwa Kutumia Kamera Hii
Niandikie hapo chini sehemu ya comment je unaisubiria kwa hamu huduma hii ikufikie katika App yako ya Facebook? Ningependa kusikia kutoka kwako.