fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Facebook Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Facebook imebadili jina na kuitwa ‘Meta’

Facebook imebadili jina na kuitwa ‘Meta’
Spread the love

Facebook imebadili jina na kuitwa ‘Meta’, uamuzi huu ulifanyika ili kutoa nafasi kwa kampuni hii kuweza kuwekeza katika teknolojia zingine. “Kampuni yetu imeshikamana sana na huduma moja kiasi kwamba haiwezi kuwakilisha kila kitu tunachofanya leo, ukiachilia mbali katika siku zijazo,” Zuckerberg alisema.

Katika mpangilio huu mpya mitandao yote ya kijamii inayomilikiwa na Facebook kama Facebook, Instagram na Whatsapp pamoja na kampuni zingine zitakuwa chini ya Meta. Uamuzi huu wa kuweka kampuni mama kwaajili ya kusimamia kampuni zingine ulifanywa pia na Google mwaka 2015 ambapo Google iliunda kampuni mama inayoitwa Alphabet ili kusimamia shughuli zake zote pamoja na makampuni yake mengine.

Facebook imebadili jina

Chapa Mpya ya Facebook ikizinduliwa Makao makuu Menlo Park, California

 

SOMA PIA  Bitcoin ni nini? Fahamu mambo yote muhimu ya kujua kuhusu Bitcoin. #Digitali #Pesa

Mmiliki wa Facebook alitangaza jina hilo jipya alipokuwa akizindua mipango ya kujenga “metaverse” – ulimwengu wa mtandaoni ambapo watu wataweza kucheza magemu, kufanya kazi na kuwasiliana katika mazingira ya mtandaoni. Mabadiliko mengine ya jina la kampuni yatatokea kwenye soko la hisa ambapo jina wakilishi litabadilika kutoka FB na kuwa MVRS mwishoni mwa mwaka huu.

SOMA PIA  Nokia 2: Simu janja mpya ya bei nafuu, yenye kukaa na chaji kwa siku mbili

Sababu zilizopelekea kampuni ya Facebook kubadili jina ni pamoja na kufululiza kwa malalamiko mbalimbali yanayohusu mtandao wa kijamii wa Facebook pamoja na Instagram kupuuzia habari potofu na maudhui hatarishi zinazosambaa katika majukwa yake.

Soma zaidi kuhusu malalamiko yanayoikabili Facebook hapa. Endelea kutembelea tovuti yetu kwa taarifa zaidi kuhusu maswala ya Teknolojia, Pia unaweza kusoma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania