fbpx

Facebook na Instagram zinapambana kudhibiti uraibu

0

Sambaza

Mitandao ya Facebook na Instagram inazindua programu mpya itakayodhibiti muda unaotumiwa na wateja wao katika mitandao hiyo.

Programu hiyo itapatikana katika ukurasa wa ‘settings’ katika mitandao yote miwili baada ya kubofya ‘Your Activity’ katika Instagram ama ‘Your Time’ katika Facebook.

kudhibiti uraibu

Kipengele cha kupambana na uraibu kwenye Instagram.

Hatua hii inakuja kufuatia malalamiko kwamba utumiaji wa muda mrefu unaweza kuathiri vibaya afya ya akili. Aidha, watumiaji sasa wataweza kuona kiwango cha muda waliotumia katika mitandao hiyo miwili na kujikumbusha muda waliofikia ili kufunga ujumbe wanaopata kwa muda fulani.

kudhibiti uraibu

Uraibu: Facebook ilichapisha andiko Desemba 2017 ambalo lilitambua athari mbaya za kutumia mtandao miongoni mwa wateja wake.

Hata hivyo, watumiaji wengi wa mitandao hiyo wamekuwa na maoni tofauti na ujio wa programu hiyo ambapo wengine wanasema itasaidia kuwazindua kupunguza matumizi ya kukaa kwa muda mrefu mtandaoni.

INAYOHUSIANA  Kivinjari cha Samsung ni maarufu! Sasa kimepakuliwa zaidi ya mara bilioni 1

Watu wengine wamepinga kwa kudai njia pekee ya mtu kuweza kudhibiti muda wa kukaa mtandaoni ni mwenyewe kuamua na si vinginevyo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.