fbpx
Facebook, Magari, Mtandao wa Kijamii, Roketi, SpaceX, Tesla

Elon Musk afuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook baada ya kujaribiwa

elon-musk-afuta-kurasa-za-spacex-na-tesla-kwenye-facebook-baada-ya-kujaribiwa
Sambaza

Mambo si mazuri kabisa kwa upande wa Facebook baada ya kukumbwa na kashfa inayopelekea watu kuanza kuukacha mtandao huo wa kijamii wenye watumiaji wengi ulimwenguni.

Mara tu Bw. Brian Acton ambaye ni mwanzilishi mwenza wa WhatsApp (hivi sasa WhatsApp ipo chini ya Facebook baada ya kununuliwa kwa $16bn) kuanzisha kampeni ya kufuta akaunti ya Facebook (#DeleteFacebook), sasa suala hilo ni maarufu sana kwenye Twitter inaonekana kupata mwitikio kutoka kwa watu wengi.

INAYOHUSIANA  Facebook inafanyia majaribio kipengele kipya kutenganisha machapisho ya kawaida na yale ya kibiashara

Elon Musk ni mmoja wa watu ambao wamefuta kurasa za SpaceX na Tesla zilizokuwa zimeshaidhinishwa (verified) baada tu ya mtu mmoja kumwambia “Afute kweli kama yeye ni mwanaume”.

kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook
Elon Musk: Alichokijibu kwenye Twitter baada ya kujaribiwa iwapo anaweza akafuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook.

Ni kitu rahisi sana kufuta ukurasa kwenye Facebook lakini ukweli ni kwamba Facebook wenyewe wamefanya imekuwa ngumu sana kuondoa kabisa ukurasa husika hata mara baada ya kile kipindi ambacho unaruhusiwa kurudisha tena ukurasa wako hewani kupita.

INAYOHUSIANA  Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi
kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook
Kufutwa kwa kurasa za SpaceX na Tesla: Hiki ndio utakachokiona baada ya kujaribu kutafuta ukurasa wa SpaceX/Tesla kwenye Facebook.

Elon Musk ameonekana mtu wa kutojali uwepo wa kurasa za mitandao ya kijamii kuhusu kile ambacho kampuni zilizopo chini yake zinazalisha. Pengine kujiamini huko kunatokana na alivyoweza kuibadilisha Tesla iliyokuwa ikionekana kampuni ambayo inaishia na kuibadilisha kabisa kwa kuifanya kuwa moja ya makampuni yenye uwekezaji mkubwa kwenye teknolojia.

Ni rahisi/vigumu kiasi gani kufuta ukurasa wa kwenye Facebook ambao unatumia/ulitumia muda mwingi kuujenga na kufikia mpaka hapo ulipo na ukizingatia kuna kashfa iliyoikumba Facebook?

Vyanzo: Gadgets 360, Vox

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Elon Musk afuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook baada ya kujaribiwa – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    March 24, 2018 at 11:12 pm

    […] post Elon Musk afuta kurasa za SpaceX na Tesla kwenye Facebook baada ya kujaribiwa appeared first on TeknoKona Teknolojia […]