fbpx

Dell XPS 15: Kompyuta nzuri kwenye uhariri wa picha/video

1

Sambaza

Uhariri wa picha/video umekuwa chanzo cha kipato kwa wakubwa na wadogo. Wengi wanaweza kudhani kuwa kompyuta zinazotengenezwa na Apple (Mac) ndio pekee nzuri sana kwenye suala zima la uhariri wa picha au picha jongefu ila zipo zinazotumia Windows ambazo nazo ni bora zaidi.

Laptop ya Dell XPS 15 ni moja ya kompyuta bora sana na iliyosifika kwa uwezo wake kiasi cha kufanya kazi za uhariri wa picha au video kupitia programu spesheli kuwa rahisi na zinazofanyika katika kiwango kizuri.

Je, Dell XPS 15 ina sifa gani zinazoifanya kuwa chaguo sahihi kwa shughuli za uhariri wa picha/video?

Hata mimi kabla ya kuandaa makala hii nilidhani kuwa kompyuta (Mac) zinazozalishwa na kampuni inayoshikilia nafasi za juu katika utengenezaji wa vifaa vya kiteknolojia, Apple ndio chaguo sahihi/bora/pekee kama mtu unajishughulisha na kazi ya uhariri wa picha jongefu/picha nyinginezo.

Dell XPS 15 ndio kompyuta bora kabisa katika masuala ya uhariri wa picha/video.

>Prosesa

Kwa mtu yeyote yule anayejua vizuri masuala ya kompyuta basi kitu cha kwanza kuangalia anapotaka kunua kompyuta aidha dukani au ambayo imekwishatumika kitu cha kwanza atakaka kujua uwezo wa prosesa (CPU) wa kompyuta husika. Dell XPS 15 ina kasi kiasi cha 2.8GHz Intel Core i7-7700HQ (quad-core yenye kasi ya mpaka 3.8GHz pamoja na 6MB cache).

>Kadi mahususi kwa ajili ya uonyeshi ang’avu wa picha

Kipengele ambacho ndio kiini katika Dell XPS 15 ndio hiki. Hakika ukiwa na kompyuta hii utakuwa unapata majibu ya kuridhisha kwa yeyote yule ambaye anajua vizuri kuchambua kompyuta kiufafanuzi zaidi. Kompyuta Dell XPS 15 inatumia Nvidia GeForce GTX 1050 (4GB GDDR5); Intel HD Graphics 630.

>RAM/Kioo

 Kiini kingine katika kompyuta yoyote yenye uwezo wa hali ya juu RAM yake ni muhimu kuwa ya kiwango cha juu na teknolojia yake basi iwe ya hivi karibuni. Kwenye Dell XPS 15 kuna 16GB DDR4 (2,400MHz). Kioo cha kwenye Dell XPS 15 kina ukubwa wa inchi 15.6 na pia ni kioo cha mguso.

INAYOHUSIANA  Ifahamu simu ya Huawei Mate X, simu nyingine ya mkunjo. #Uchambuzi

>Dski ujazo/Kamera

Sifa nyingine kwa kompyuta yoyote yenye uwezo wa hali ya juu inakuwa na diski ujazo wa angalau kuanzia GB 500 na kwenye hii komyuta inayofaa zaidi kwenye shughuli za uhariri wa picha na video ina GB 512. SSD- teknolojia ya SSD ni nzuri sana na inafanya shughuli kama rendering kwa haraka sana. Kamera (webcam) yake ina ubora wa 720p yenye uwezo wa kurekodi video kwa kiwango cha 4K.

Dell XPS 15 ina fingerprint, USB 3.0/USB-C, Bluetooth 4.1 na uzito wa Kg 1.8.

Kwa maelezo ya hapo juu nadiriki kusema Dell XPS 15 ndio chaguo sahihi iwapo unahitaji kompyuta mahususi kwa ajili ya shughuli za uhariri wa picha au hata uchezaji wa magemu ya ubora wa juu.

Bei yake ni kuanzia $999 (Tsh. 2,224,750) kwa yenye core i3 na kioo chake sio cha mguso.

Vyanzo: The guardian, TechRadar

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|