Data za WhatsApp kupitia Facebook, hilo ndilo badiliko jipya ambalo linatokea kwa watumiaji wote wa app ya WhatsApp duniani kote. Ni badiliko kubwa kwani kabla app hiyo ilikuwa haikusanyi data kwa kiwango hicho.
Kampuni ya Facebook kwa muda mrefu imekuwa ikitafuta njia za kutengeneza pesa kupitia app ya WhatsApp na baada ya muda mrefu wameweza kupata njia ya kufanikisho hilo.

Kwa sasa biashara zinaweza kuwa na akaunti spesheli za WhatsApp, na Facebook wanaendelea kuhakikisha akaunti hizi za kibiashara na binafsi ziweze kuwa na data za kuunganisha na utumiaji wao wa Facebook. Kama wewe ni mtumiaji wa WhatsApp, je ukiwa Facebook au Instagram unatumia akaunti gani? – Kwa kuweza kupata umoja huu katika data za watumiaji basi Facebook kupitia huduma zao za kimatangazo wataweza kuboresha ufanisi wa matangazo yao na kuboresha huduma za kibiashara kwa watumiaji wa Facebook kwa ajili ya matangazo.
Makuu yanayobadilika:
Bado WhatsApp itaendelea kutumia teknolojia ya usalama data ya ‘end-to-end encryption’, teknolojia inayohakikisha ujumbe wako hauwezi kusomwa ukitoka kwenye simu yako, na utaweza kusomwa tuu pale utakapomfikia unayemtumia.
Kwa sasa app ya WhatsApp itakuwa inachukua data kuhusu aina ya simu unatumia, kiwango cha betri, lugha, ulipo, anuani ya IP ya kifaa chako, mtandao wa simu, na data zingine muhimu kuhusu app za kampuni ya Facebook ulizonazo kwenye simu yako; kama Facebook, Instagram na Messenger.
Data hizo zitatumwa kwenda Facebook, na zinaweza kutumiwa kwa ajili ya huduma za matangazo n.k.

Watu wengi hawajafurahishwa kwani maneno yaliyotumika katika makubaliano mapya ya wateja wa WhatsApp yatamaanisha hadi namba yako ya simu ya akaunti ya WhatsApp, na data kuhusu huduma za kibiashara unazowasiliana nazo kupitia WhatsApp zitatumwa pia kwenda Facebook.
Kwa muda mrefu wapenda usalama wa data wengi walipingwa kuuzwa kwa WhatsApp kwenda Facebook, wakiamini Facebook watakuja kutumia data za watumiaji wa app hiyo kwenye huduma zao za kimatangazo – hili linaonekana limetimia.
Je unaweza kufanya nini kama hupendi suala hili?
Ni vigumu, app pekee inayokuja kwa kasi na ambayo ipo salama kwa eneo la data – aiendeshwi kibiashara data – ni Telegram. Ila kwa mataifa yetu ya Afrika Mashariki bado utumiaji wa Telegram unakua kwa kasi ndogo.
Soma Pia –Â Progamu ipi ya kutuma ujumbe ni bora kwako? Whatsapp au Telegram?
No Comment! Be the first one.