fbpx

Uchambuzi: Dash Cam ya Pro User; Kamera za kisasa kwa matumizi mbalimbali

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Siyo mara ya kwanza kuzungumzia Dash Cam na umuhimu wake kwa waendesha magari hapa teknokona. Leo tunakuletea moja-kwa-moja uchambuzi wa Dash Cam na hasa za Pro User ambazo tumebahatika kuwa nazo.

Kwa nini uwe na Dash Cam?

Jambo la msingi kujua siku zote ni kwanini ujue kuhusu kitu fulani? Dash cam zinatumika kutoa ushahidi wa ajali na matukio yanayotokea barabarani na hata gari linapokuwa kwenye maeneo ya maegesho ya magari.

Shahidi hizi zinaweza kutumika kwa ajili ya kupata marejesho ya bima kwa haraka na zinawezesha usaidizi wa kisheria kutoka kwa polisi wa usalama barabarani. Dash Cam zenye uwezo wa kutambua vitu vinavyokuja karibu zinaweza kuwezesha ulinzi wa magari kwa saa 24.

Faida za ziada

Unaweza kutumia Dash Cam kurekodi safari yako, iwe ya mikoani au mizunguko ya hapa na pale kuweka kumbukumbu. Hii ni njema sana kwa wale wanaoenda kwenye maeneo yenye sifa za kuwa na uzuri wa kipekee.

INAYOHUSIANA  Huawei P30: Hizi hapa simu mbili mpya za Huawei za P30 na P30 Pro

Hii inakuwezesha kushirikisha watu mbalimbali kuhusu matukio ya aina tofauti yanayotokea barabarani. Unaweza kutumia Dash Cam kufuatilia mienendo ya wafanyakazi wako (madereva wa kampuni).

Kuna ubaya wa kuwa na Dash Cam?

Zipo nchi ambazo hukataza matumizi ya Dash Cam kwa mfano, Ujerumani na majimbo kadhaa ya Marekani kwa sababu za kulinda faragha ya watu kwenye maeneo ya kadamnasi na kwenye mitandao. Kwa maana hiyo, ni vyema kuangalia sheria za nchi husika kabla ya kutumia Dash Cam barabarani. Hapa kwetu Tanzania na Afrika ya mashariki kwa ujumla, hamna sheria inayokataza kutumia Dash Cam ila itakubidi uwe muangalifu kwenye matumizi ya video zake mtandaoni, kwamba zisiwe za kuumiza hisia za watu wengine.

Undani wa Dash Cam za Pro User

Kama ungependa kumiliki Dash Cam kwa ajili yako au kwa ajili ya kampuni, Dash Cam iliyokuwa sokoni sasa inaitwa Pro User Cam.

Yaliyomo kwenye boksi: Kamera ya kurekodi, Kishikio, Charger ya kwenye gari, Waya wa Micro-USB kwenda kwenye USD

Sifa zake

  • Uwezo kurekodi video
INAYOHUSIANA  Infinix ZERO 6 imekuja na Teknolojia Ya AI (Artificial Intelligence) Nchini! #Tanzania

Dash Cam ya Pro User ina uwezo mkubwa wa kurekodi picha za hali ya juu (Hadi 1080FHD 1920×1080); hii ikimaanisha kuwa utaweza kuona vitu mbalimbali na maandishi kwa urahisi na kwa umakini Zaidi.

Tazama muonekano wa rekodi yake: Tazama video

  • Kupiga picha

Kwa kutumia Dash Cam hii unaweza kupiga picha zinazoweza kuwa kama kumbukumbu yako ya maeneo yaliyokuvutia zaidi. Picha hizi ni za ukubwa zaidi ya kamera za kawaida za simu (hadi 12MP).

Kamera ya Dash Cam Pro

  • Mipangilio/Settings (Vipengele) ya kipekee
    • G-sensor: Kati ya mambo yanayofurahisha Zaidi kwenye Dash Cam ya Pro User ni uwezo wa kugundua kama kuna mtu au kitu kinachotembea mbele au nyuma ya gari. Hii ina maana kwamba Dash Cam inaweza kuwekwa kwenye hali ya usingizi wakati hamna purukushani lakini punde tu mtu atakaposogelea gari, Dash Cam inaanza kurekodi na kukupa uwezo wa kuona mtu aliyeisogelea gari na amefanya nini. Hii ni habari njema kwa watu wanaopenda ulinzi wa magari yao pale linapokuwa kwenye eneo la maegesho.
    • Parking mode: inawezesha Dash Cam kuweza kurekodi matukio punde tu gari likipata mshituko (kutokana na kugongwa) au linapohamishwa pale linapokuwa kwenye eneo la maegesho.
INAYOHUSIANA  Undani wa Sony Xperia Ace #Uchambuzi

Pengine jambo la ziada la kushauri kuhusu Dash Cam hii ni kwamba inahitaji kufanya kazi na memori kadi ya kuanzia GB 1 ambayo itabidi ununue na bei ya Dash Cam yenyewe pekee ni Tsh. 75,000/=.

Kwa kifupi, hiyo ndiyo Dash Cam ya Pro User na uwezo wake. Kuweza kupata Dash Cam yako, piga simu namba +255 754 006306 au barua-pepe info@ststanzania.com na ujipatie sasa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comments are closed.