fbpx

Intaneti, Teknolojia, Usalama

Dark Web ni nini? Fahamu zaidi kuhusu mtandao huu wa siri na tovuti zake

dark-web-ni-nini-fahamu-zaidi-kuhusu-mtandao-wa-siri

Sambaza

Kwenye masuala ya kuperuzi unaweza kutumia njia mbalimbali ili tu kutimiza adhama. Kwa mantiki hiyo mtu anaweza kutumia “Rasmi” au akaamua “Kujificha”.

“Dark web” ni nini?

Dark Web inahusisha tovuti za mtandao ambazo hazitambuliki kwa injini za utafutaji za kawaida; kwa maana ya kwamba mfumo wa tovuti ambao haupo katika mfumo rasmi wa WWW (World Wide Web) na njia nyingine inayoweza kupatikana kwa urahisi kwa kompyuta zilizo kwenye unganisho moja la mtandao (network).

Tovuti nyingi katika mfumo wa Dark Web zinajumuisha kuwa na mfumo wa siri wa mawasiliano na utumaji data na usalama wa mfumo mkuu wa utunzaji data wa tovuti husika – database. Tovuti hizi haziwezi kupatikana kupitia vivinjari vya kawaida – Chrome, Opera, Firefox n.k.

INAYOHUSIANA  Apple Watch yasaidia kuokoa maisha ya binadamu
dark web ni nini
Dark Web ni nini? – Mitandao imegawanywa katika familia tatu, wa kwanza ndio uliozoeleka wa mitandao mbalimbali ya kijamii, habari n.k inayoweza kufikiwa na mtu yeyote. Ya pili, ni deep web ambayo ni ile mitandao inayohusisha watu kuwa na logins spesheli – hii ni ile ya makampuni binafsi, mabenki au ya kiserikali. Mtu wa kawaida haweza ata kufahamu kama ipo. Na familia ya tatu ndio hii ya Dark Web. Hii inahusisha tovuti ambazo zina usiri mkubwa na utahitaji kivinjari spesheli ili kuweza kutembelea tovuti zake.

 

Vivinjari Maalumu kama vile TOR BROWSER vinatakiwa kutumika ili kukuwezesha kufikia tovuti zilizo kwenye mfumo wa Dark Web. Tovuti nyingi za dark web hutoa huduma za kiwango za mtandao kwa usiri zaidi, ambazo hufaidisha wanasiasa na watu ambao hujaribu kufanya hali ya matibabu kuwa faragha.

Kwa bahati mbaya, masoko ya madawa ya kulevya na shughuli zingine za kijinai hufaidika zaidi katika mtandao huu wa Dark Web.

INAYOHUSIANA  Simu milioni 900 za Android hatarini kudukuliwa
tovuti za dark web
Kwenye Dark Web kuna hadi tovuti za kijamii, badala ya kutumia anuani za .com n.k, anuani inayotumia kwenye tovuti hizi ni .onion

 

Dark Web imejipatia sifa mbaya na kutambulika na watu kama ‘bandari ya shughuli haramu’.

Hulaumiwa mara kwa mara kwa maovu yanayofanyika na watumiaji wake, kama unyanyasaji/uzalilishaji wa watoto kupitia mtandao na uwezo wa watu kukodi watu wa kufanya mauaji. Hata hivyo, uhalifu huu ulikuwepo tangu zamani hata kabla ya intaneti na dark web. Dark web inapelekea ugumu katika ufuatiliaji na ukamataji wa wavunjifu wa sheria.

FAIDA za DARK WEB

Dark web inasaidia watu kudumisha faragha na kutoa maoni yao kwa uhuru. Faragha/Usiri ni muhimu kwa watu wengi wasio na hatia ambao hutishwa na wanyang’anyi na wahalifu wengine wengi. Mwishowe, umaarufu wa dark web na wahalifu unatengeneza njia nzuri kwa maafisa siri wa polisi kuwasiliana.

INAYOHUSIANA  Teknolojia ya magari ya umeme yaingia Serengeti

HASARA za DARK WEB

Dark Web inaweza kurahisisha kutendeka kwa uhalifu mbaya sana. Wakati mfumo huu wa mtandao unahahidi faragha kwa watumiaji wake, pia unaweza kutumika katika kukiuka faragha za watu wengine. Picha za siri, rekodi za afya, na habari za kifedha zimekuwa zikiibwa na kuuzwa au kupatikana kwa bure kupitia tovuti zinazopatikana kwenye mfumo wa huu wa mtandao.

Je una nini kingine ungependa kufahamu kuhusu tovuti za Dark Web? Tuambie kwenye comment.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Dennis Dealma

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*