fbpx
Apple, Roboti

Daisy: Roboti wa Apple anayefumua simu 200 ndani ya lisaa

daisy-roboti-wa-apple-anayefumua-simu
Sambaza

Apple wametambulisha roboti yao waliyoipa jina la Daisy. Roboti huyo anauweza wa kufumua simu 200 ndani ya muda wa saa moja.

Roboti huyu anasaidia mpango mzima wa Apple wa kusaidia mazingira, kwani baadhi ya vipuli vinavyokuwa kwenye simu vinaweza kutumika tena (recycled).

Ndani ya simu janja za kisasa kuna vitu mbalimbali vyenye thamani kubwa, hii ni pamoja na vipuli vilivyotengenezwa kwa kutumia madini kama vile dhahabu, shaba, platinum, lithium, na mengine mengi. Vipuli hivyo vinaweza kuyeyushwa na kwa kutumia madini hayo kutengeneza tena upya vipuli vingine.

INAYOHUSIANA  Zifahamu Keyboard 5 Za Mbadala Kwa Ajili Ya iPhone!
roboti wa apple daisy
Simu zikiwa zimewekwa kwenye mkanda wa kupokelewa na roboti Daisy

Roboti Daisy ataweza kutambua aina ya iPhone na kisha kupitia data alizowekewa kuweza kufahamu jinsi vipuli vimepangwa ndani ya simu hiyo na hivyo kuweza kuvifungua vyote kwa usahihi.

roboti daisy iphone
Vipuli mbalimbali vya ndani ya simu za iPhone vikiwa vimekwishatolewa na roboti huyo

‘Kwa kila simu 100,000 za iPhone roboti Daisy ataweza kupata kilo 1,900 za alumini, kilo 710 za shaba.’

Apple wanalenga kuweka roboti hao katika miji mbalimbali ya nchini Marekani na kuendelea kutoa punguzo la bei kwa watu watakaoleta iPhone zilizotumika wakati wanataka kununua mpya.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |