fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao

CNN Kuja Na CNN Plus! #2022

CNN Kuja Na CNN Plus! #2022

Spread the love

 Cable News Network (CNN) imesema mpaka kufikia mwaka 2022 itakua imeshaanzisha huduma mpya ambayo itajulikana kama CNN Plus nahuduma hii itakua ni ya ku’stream

Ni wazi kuwa siku hizi huduma za Ku’stream zimekua ni nyingi sana na hivyo pengine labda mtandao wa habari wa CNN umeona unabaki nyuma nyuma sana.

CNN

CNN

CNN mpaka sasa hawajaweka wazi kwamba huduma hiyo itakua inapatikana kwa gharama gani lakini wamegusia kidogo kwamba inaweza ikahusisha vipindi vya zamani vilivyokuwa na majina makubwa makubwa.

Baada ya kuanzishwa kwake ndani ya miezi sita mpaka tisa ina mpango wa kuajiri wafanyakazi 450. Ukiachana na hayo vile vile huduma itahusisha vipindi vile vya ‘live’ na vile vinavyopendekezwa sana na watazamaji n.k.

CNN wamesema kwamba wakati CNN plus inatambulishwa, huduma hiyo kwa mwanzo haitahusisha matangazo lakini hawakuweka wazi kuwa mbeleni itakuawaje.

Moja Ya Studio Ya CNN

Moja Ya Studio Ya CNN

Kingine katika uzinduzi usitegemee kuwa CNN Plus itakua inajitegemea na App yake, la hashaaa… App ile ile ya CNN itakuwa inatumika na wale ambao wanataka kuingia katika CNN Plus, ila lazima kuwe na taratibu za kufanya hivyo.

SOMA PIA  FAHAMU 'End-to-End Encryption' Ni Nini, Na Ina Maana Gani?

Japokuwa kwa haraharaka unaweza sema CNN Plus mbona ina kila namna ya kufanana na CNN kwa kila kitu, lakini wenyewe wanasema kuwa kutakuwa na tofauti kedekede.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, Hii umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania