Britney Spears ni mmoja kati ya wasanii wakubwa sana duniani wa muziki wa miondoko aina ya pop, pia mwanamuziki huyu ana washabiki wengi sana.
Mwanamuziki amechukua maamuzi ya kusema kuwa anataka kuanzisha App ya mtandao wa kijamii ambayo itakua kama ni ngazi kati yake na mashabiki wake wa dhati
App hii itakuwa ikitumika na mashabiki zake katika kumuuliza maswali ya moja kwa moja licha ya hivyo pia itakuwa ni njia nzuri kati ya yeye na mashabiki zake kuwa pamoja.
Kampuni nguli ya kutengeneza magemu hapo mwanzoni ilitengeneza mchezo ulioitwa Britney Spears: American Dream na toleo lilitoka kwa wale watumiaji wa iOS na Android.

Mchezo huu ulikuwa unachezwa kwa watu kuanza katika hali ya chini/ kuwa hawajulikani mpaka kufikia katika hatua ya kuwa wasanii wakubwa katika miondoko ya pop (kama Britney Spears).
Britney amesema kuwa App hiyo itakuja hivi karibuni tuu. Na watu wasishangae sana kwani hii haitakuja kwa njia ya gemu kama lile la mara ya kwanza. Hapa watu wataweza kuongea na kujichanganya na msanii huyo.

Britney alisema kwa siku anakutana na watu wengi sana akiwa kama msanii, mara nyingi anapiga nao picha. Watu hao kwa kiasi kukubwa humuelezea jinsi wanavyomkubali na kumuonyesha vitu vingine mbalimbali. Hivyo basi anaheshimu sana jambo hilo na anataka aweze kuwa karibu na mashabiki zake wa dhati wote.
Je wewe unaona ni sahahi kwa msanii kuanzisha App ili mradi awe karibu zaidi na mashabiki zake? Ningependa kusikia kutoka kwako. Acha mawazo yako hapo chini sehemu ya comment.