Kwa miaka miwili sasa kampuni ijulikanayo kama Blackberry imekuwa ikipata hasara katika uuzaji wa simu janja kutoka kampuni hiyo.
Kwa zaidi ya miaka miwili Blackberry imekuwa ikipata hasara. Blackberry ni kampuni maarufu sana kwa utengenezaji wa simu janja, ni kampuni kutoka Canada na imeripotiwa kuwa Blackberry wamepata hasara ya dola milioni 670 katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Hata hivyo katika matoleo ya simu janja za Blackberry zilizotoka hivi karibuni waliamua kutumia programu endeshaji ya Android bado simu zao hazifanyi vizuri katika mauzo, simu za BlackBerry kwa sasa zinashikilia chini ya asilimia 1 ya soko la dunia.

Asilimia kubwa ya mapato wanayopata yanatokana na utengenezaji wa programu endeshaji ambazo zinatumika katika mambo ya kiusalama na hivyo kama kampuni wanafikiria kuachana na biashara ya utengenezaji wa simu janja na kuzidi kuwekeza zaidi kwenye biashara inawaingizia faida zaidi badala ya kuedelea kupata hasara.
Je, wewe ni mpenzi wa simu janja kutoka Blackberry? Tuambie nini maoni yako kuhusiana na uamuzi ambao Blackberry wanataka kuuchukua? Endelea kufuatilia kutoka hapahapa Teknokona nasi tutazidi kukuhabarisha.
Chanzo: Telegraph, BBC