fbpx
Android, apps, iOS, Teknolojia

BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31

blackberry-messenger-bbm-kufungwa-mei-31
Sambaza

Teknolojia inakuwa na mabo yanabadilika kitu ambacho kinasababisha makampuni kuacha kutoa huduma fulani na kwa wale amabao tulishawahi kutumia simu za BlackBerrry na hata simu za Android tutakuwa tunafahamu vyema kuhusu BlackBerry Messenger (BBM) lakini sasa kufikia tamati ya matumizi Mei 31 2019.

Hapo  awali kabisa hudua ya mawasiliano kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi/simu, BBM ilikuwa ikipatikana kwa wenye BlackBerry pekee na mwaka 2013 mwishoni watumiaji wa BBM kwenye BlackBery wakawa wanapata changamoto ya kuwasiliana kwa ndio hapo ilipoanza kupatikana kwenye iOS na Android.

Historia ya BlackBerry Messenger (BBM) kwa ufupi

Programu hii ilitengenezwa na BlackBerry LTD mwaka 2005 na kuachiwa kutumiwa Agosti 1 2005. Mwaka 2016, Emtek-kampuni inajihusisha na masuala ya teknolojia yenye makazi yake Indonesia ikanunua leseni ya BBM kutoka kwa BlackBerry LTD. Aprili 2016, 87.5% ya watumiaji wa simu za Android nchini Indonesia walikuwa wamehifadhi programu hiyo.

Mawasiliano baina ya watu na watu yanaunganishwa na ‘BlackBerry PIN‘ ambapo mwanzoni mwa mwaka 2013 BlackBerry walikuwa wakitumia 30PB (zaidi ya GB 30 milioni) zilitumika kila mwezi kufanikisha mawasiliano, mpaka kufikia mwishoi mwa mwaka huo-2013 vikatuni (stickers) zipatavyo tisini milioni zilikuwa zimesambazwa, simu 150 elfu zilikuwa zimepigwa na mpaka kufikia mwaka 2015 BBM watumiaji wake walifikia 190 milioni.

BlackBerry Messenger
BlackBerry Messanger inatarajiwa kusitishwa matumizi mnamo Mei 31 ambapo mtumiaji aliweza kutuma kitu chenye ukubwa usiozidi MB 16.

Kwanini BBM itafungwa Mei 31?

Kwa miaka hii ya karibuni ni watu wachache ambao wanavutia/kutumia BBM kwa maana ya kwamba wengi wao wamehamia kwenye programu tumishi nyinginezo na hata wale ambao wanataka kutumia BlackBerry Messenger wanapata wakati mgumu kuingia kwenye akauni zao LAKINI BlackBerry wataiacha BlackBerry Enterprise (BBM Me) kwa Android na iOS ikipatikana BURE kwa kipindi cha mwaka mmoja kisha baada ya hapo watumiaji wake (kampuni) itakuwa ikilipia $2.49/miezi sita (zaidi ya Tsh. 5,800).

INAYOHUSIANA  Drones za Amazon zinazotumika kusambaza vitu kwa wateja

Hakuna chenye mwanzo kisichokuwa na mwisho na ndio hivyo wahusika wamedikia maamuzi ya kuachana na BlackBerry Messenger mnamo Mei 31 ya mwaka huu. Je, wewe ulikuwa ni mmoja wa watumiaji wazuri wa BBM?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|