BlackBerry wanaonesha ni kwa jinsi gani bado hawakubali kuanguka katika eneo la biashara za simu, tayari wamejiweka tayari kuja tena na simu nyingine tatu tofauti zinazotumia Android hivi karibuni.
Ingawa kumekuwa na habari mara kadhaa kutoka vyanzo mbalimbali ya kwamba BlackBerry wanaamua kuachana na biashara ya utengenezaji simu wenyewe ndio kwanza wameingia jikoni na kujiandaa kuja na vitu vipya.
Vyanzo mbalimbali vimeonesha BlackBerry kuja tena na simu 3, zinazoonekana zitakuwa na angalau kwenye bei za kiushindani ukilinganisha na simu walizoziletwa kwa sasa. Mfano BlackBerry Priv.
Imeshaonekana itakuwa vigumu kwa BlackBerry kurudi tena kwenye soko la uuzaji simu kama watakuja kwa njia ya kushindana katika suala la bei na simu kama za iPhone au simu za Samsung za familia ya Galaxy S. Mafanikio kwa BlackBerry kwa sasa yatategemea pia wao kuweza kuleta simu zenye bei inayoweza fikiwa na watumiaji wengi.
Kwanza kabisa kuna BlackBerry Neon
Hii ni simu inayotegemewa kuwa si ya bei ghari sana. Inaachana na uwepo wa keyboard na badala yake itategemea kioo cha HD cha mguso (touchscreen) cha ukubwa wa inchi 5.2.
- Inakuja na body la aluminuium na prosesa ya Qualcomm Snapdragon 617,
- RAM GB 3
- Diski ujazo (storage) wa GB 16
- Betri la ujazo wa mAh 2,610
Sifa zingine bado hazijatolewa rasmi ila inategemewa inaweza ikawa na kamera ya MP 13 na huku kamera ya selfi ikiwa na megapixel 8.
Inategemewa kutambulishwa rasmi mwezi wa nane mwaka huu.
Simu ya pili ni BlackBerry Argon
Hii inategemewa kuingia sokoni mwezi wa kumi mwaka huu. Pia kama BlackBerry Neon haitakuwa na keyboard.
BlackBerry Argon itakuja na kioo cha touch cha inchi 5.5 cha kiwango cha juu cha HD – QHD resolution (Hicho ndicho kilichokuwa kimetumika kwenye BlackBerry Priv).
Simu hii inawalenga watu wa hadhi ya kati zaidi – kama watu wanaotumia kikazi.
Sifa zinginezo;
- Kioo cha inchi 5.5 (2560×1440 QHD)
- Prosesa – Snapdragon 820
- RAM GB 4
- Diski uhifadhi (storage) – GB 32
- Betri – mAh 3,000
Pia inakuja na uwezo wa fingerprint sensor, USB Type C, na kamera ya megapixel 21 na huku ya selfi ikiwa MP 8.
BlackBerry Mercury

Simu hii inategemewa kuja mwanzoni mwa mwaka 2017.
BlackBerry Mercury itakuwa na keyboard.
Bodi yake itakuwa ya aluminium na kioo chake cha HD kitakuwa na ukubwa wa inchi 4.5.
Sifa zingine
- Prosesa Qualcomm Snapdragon 625
- RAM GB 3
- Diski uhifadhi (Storage) – GB 32
- Ujazo wa betri – mAh 3400
- Kamera – Megapixel 18, selfi MP 8
Je watafanikiwa?
Kwa kiasi kikubwa simu hizi ndio zitaonesha kama BlackBerry bado wanauwezo wa kurudi tena. Kwa sasa wamejitahidid kwani simu hizi zinaonekana zitaweza patikana kwa bei inayoweza fikiwa na wengi ukilinganisha na simu za BlackBerry walizozileta tayari – mfano BlackBerry Priv.
Tuambie unaonaje uwezo wa simu hizi? Tutaendelea kufuatilia ujio wa simu hizi na tutakupatia taarifa zaidi.
Vyanzo: Makala hii imeandikwa kwa kutumia vyanzo mbalimbali – VentureBeat.com, TheInquirer n.k
One Comment
Comments are closed.