Ingawa tayari walishatangaza rasmi kuachana na biashara ya utengenezaji simu, kampuni ya BlackBerry imetoa taarifa rasmi ikisema bado wanasimu yao ya mwisho kwa ajili ya kuingia sokoni.
Mkurugenzi wa kampuni ya BlackBerry bwana Chen, alikaririwa na Bloomberg TV akisema “Tunayo simu moja yenye mfumo wa keyboard ambayo tuliwaahidi watu. Inakuja.”

Simu hiyo itakuwa na kioo cha mguso (touch) pia itakuja na eneo la keyboard maarufu za QWERTY ambazo ni maarufu kwa simu za BlackBerry.
Kulingana na mtandao wa GSMArena simu hiyo itakuja na sifa zifuatazo;
- Itatumia Android 7.0
- Display ya inchi 4.5 HD
- Kamera ya megapixel 18, ya selfi itakuwa ya megapixel 8.
- Betri la mAh 3,400
- Prosesa ya Snapdragon 625 CPU ikiwa na RAM ya GB 3
- Kiwango cha diski ujazo wa GB 32
Ingawa taarifa za bei bado hazijatoka rasmi simu hiyo inalenga watumiaji wa hali ya kati na inategemewa kutambulishwa rasmi na kuingia sokoni kati ya mwishoni kabisa wa mwaka huu au kipindi cha mwanzo cha mwaka 2017.