Black Friday ni nini? Ijumaa Nyeusi ama Black Friday kama inavyoitwa kwa kimombo, ni Ijumaa ya kwanza baada ya sikukuu ya Kikristo ya mavuno ama Thanksgiving inayosheherekewa zaidi huko Marekani.
Kwa mwaka 2020 siku hii ya Black Friday itasheherekewa Ijumaa hii yaani tarehe 27. Siku hii itanguliwa na siku ya Mavuno ama Thanksgiving ambayo mwaka huu itafanyika tarehe 26 yaani Alhamisi hii.
Black Friday pamoja na yote huashiria kuanzaa kwa msimu wa manunuzi wa Christmas. Siku hii inatajwa kuwa ndiyo siku pekee ambayo inaongoza kwa manunuzi mengi zaidi nchini Marekani. Kuongeza hamasa ya wanunuzi maduka na wauzaji wengi wa rejareja hutoa punguzo kubwa la bei siku hii, kutokana na punguzo la bei watu wengi huvutiwa kufanya manunuzi katika siku hii.
Kama inavyokuwa hapa kwetu wakati wa msimu wa Sabasaba ambapo wafanyabiashara wengi hupunguza bei za bidhaa basi pia hata Marekani wakati wa wikiendi ya Thanksgiving biashara nyingi hupunguza bei ya bidhaa zao.
Soma Pia – Kwa ushirikiano na MasterCard, sasa lipia malipo ya mtandaoni kwa kupitia M-Pesa
Siku hii imekuwa ni siku ambayo yenye mauzo mengi kwa mfululizo toka mwaka 2005. Ingawa umuhimu wa siku hii umekuwa ukipungua kutokana na wafanya biashara wengi kuweka punguzo sio tu kwa siku hii bali kipindi chote cha Novemba na Disemba.
Jina Black Friday lilikuwa linatumiwa na polisi huko Philadelphia, ambao waliita siku hii Ijumaa Nyeusi kuashiria foleni kubwa ya magari pamoja na watembea kwa miguu. Ingawa baadaye maelezo ya maana ya jina hili yamebadilika na kuashiria wakati ambao wafanya biashara huanza kupata faida.
Jumatatu inayofuata baada ya Black Friday inajulikana kama Cyber Monday. Cyber Monday ni kama ilivyo Black Friday isipokua manunuzi katika siku hii yanakuwa ya kimtandao zaidi.
Biashara nyingi zinazo uza bidhaa mitandaoni hutoa punguzo kubwa la bei siku hii. Hii inawapa watu hamasa zaidi kununua bidhaa mtandaoni siku hii.
Hapa nyumbani Tanzania zipo kampuni mbalimbali ambazo zimekua zikitoa punguzo kufuata sherehe hizi. Ingawa ufahamu na muamko sio mkubwa kama ilivyo Marekani au baadhi ya nchi za barani Ulaya.
Je wewe unafuatilia siku hizi? kama ndiyo tuambie maduka ambayo yanatua punguzo la bei kipindi hiki.
Chanzo: Wikipedia.com
No Comment! Be the first one.