fbpx
Teknolojia

Bill Gates na mpango ya kujenga jiji janja kwenye jangwa

bill-gates-na-mpango-ya-kujenga-jiji-janja-kwenye-jangwa
Sambaza

Ulimwengu wa teknolojia sasa unaenda kwenye upande wa kuwa na majiji janja ambayo yatakuwa ymejaa na huduma mbalimbali za jamii pamoja na za kuimarisha uchumi wa eneo husika.

Tajiri nambari moja ulimwenguni kupitia moja kampuni zake ameamua kuwekeza mamilioni kwenye ujenzi wa jiji janja nje kidogo ya Phoenix, Arizona-Marekani.

Hivi karibuni imebanika kuwa wawekezaji wenza na Bw. Bill Gates walilipa karibu $80 milioni kuweza kukununua eneo lenye ukubwa wa ekari takribani 24,800 nje kidogo ya Phoenix sehemu iitwayo Belmount.

Dhima kuu ni kutengeneza jiji ambalo litawaunganisha wakazi wake kwa mawasiliano, miundombinu, teknolojia za hali ya juu sana ikiwemo teknolojia mpya zinazoibuka na matumizi ya magari yanajiendesha, na teknolojia zinazofanana na hizo.

Kitakachojengwa kwenye jangwa na baadae kubalika na kuwa ‘jiji janja’.

Belmount ambao kwa sasa eneo hilo ni kama jangwa linatarajiwa kubadilishwa kabisa kwa ujenzi wa  jiji janja litakalokuwa na majengo mbalimbali kama vile:-

  • nyumba za makazi takribani 80 elfu,
  • eneo la ekari 3,800 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, ofisi na mahali pa kuuzia vitu kwa rejareja,
  • ekari 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule za umma huku karibu ekari 3,400 zikibaki kama eneo la wazi.

Jiji hilo janja litakalojengwa linatarajiwa kuweka njia huru kutoka Reno mpaka Mexico huku ikiunganishwa kwa pamoja miji ya Phoenix na Las Vegas. 

Mfano wa jiji janja.

Wakosoaji mbalimbali ambao wameuangazia mpango wa Bw. Bill Gates na washirika wenza wanaamini ili mji uwe mzuri ni vyema ukajengwa majengo ambayo watu wengi wataweza kuyamudu kuyalipia, sehemu za starehe lakini wanaohusika na uundaji wa jiji hilo vitu hivyo hajaviangazia.

Vyanzo: Fortune, SmartCitiesDIVE

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Programu wezeshaji inayoweza kujua unachofikiria
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|