fbpx

Apple, IPhone, simu, Teknolojia

Bidhaa za Apple zitakazotoka Septemba-Oktoba 2020

bidhaa-za-apple-zitakazotoka-septemba-oktoba-2020

Sambaza

Mwezi Septemba unafahamika kwa Apple kutoa bidhaa nyingi na uzinduzi wa vifaa vya kidjiti. Tayari kupitia vyanzo vya kuaminika imeshajulikana tutegemee kuona nini.

Moja ya bidhaa ambayo watu wengi kutoka mataifa mengi duniani wanasubiri ni ujio wa iPhone 12 pamoja na washirika wake kutoka familia moja wanataamiwa kuonekana kinagaubaga mwezi Septemba mwaka huu na kwa mujibu wa akaunti ya Twitter, Bw. Jon Prosser aliyekuwa ameandika kuhusu iPhone SE 2020 na ikawa na tarehe ikawa ni ileile ameweka wazi kuhusu tarehe ya uzinduzi pamoja na kuingia sokoni kwa bidhaa za Apple mwezi Septemba. Mtiririko wake ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Uber kufanya Majaribio magari Yanayojiendesha yenyewe

Apple Watch 6 na iPad 10.2

Kwa mujibu wa Bw. Jon Prosser bidhaa hizi zitazinduliwa Septemba 7 bila ya chereko lakini hatazitambulisha mbele ya waandishi wa habari.

iPhone 12 na iPhone 12 Pro

Bidhaa hizi zitafanyiwa uzinduzi ambao unatazamiwa kufanyika Oktoba 12 pamoja na kuiagiza kabla ya kuingia sokoni halfu wiki moja baadae (yaani Oktoba 19) iPhone 12 itangia sokoni huku iPhone 12 Pro ikitazamiwa kwenda kwenye mauzo mwezi Novemba. Utakumbuka kuwa tulishawahabarisha kuhusu iPhone za Septemba kuchelewa kuzinduliwa.

INAYOHUSIANA  Kifaa cha kupima malaria bila ya damu chaundwa nchini Uganda
Septemba-Oktoba
Taarifa kuhusu ni lini bidhaa za Apple kwa mwezi Septemba-Oktoba zitatoka.

Kuhusu ujio wa iPhone toleo la 12 tutegemee kuona iPhone 12, iPhone 12 Max, iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max. Mwezi Septemba-Oktoba si mbali kutoka sasa kwahiyo tukae tayari na TeknoKona tutawahabarisha kuhusu uzinduzi huo pamoja na mambo mengine.

Vyanzo: MacRumours, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|