Anguko la Nokia duniani. Ni kwanini ilianguka? Fahamu zaidi
Baada ya kufanikiwa kuliteka na kulimiliki soko kwa takribani muongo mmoja ghafla taratibu mauzo yanapungua na kuanguka kabisa sokoni. Inashangaza na kushtua kidogo kuona kampuni kubwa ya simu ya Nokia iliyojizolea umaarufu mkubwa sana duniani ikitapatapa walau kupata asilimia ndogo tu yaani angalau asilimia moja ya sehemu ya soko la simu janja duniani!.