Unakumbuka kuna kipindi ulikua unaweza kuona asilimia ya chaji iliyobakia katika iphone yako katika ‘status bar’? hali hii ilikuja ikatoweka kwa baadhi ya iPhone.
Kwa kifupi ni kwamba kuanzia katika iPhone X na kuendelea huduma hii ilihamishwa katika eneo amablo tulikua tumelizoea.
Kwa kuanzia katika iPhone X na kuendelea huduma hii ilikua ikipatikana katika sehemu ya control centre –sehemu ambayo tunaweza kuwasha tochi, Wifi, Bluetooth, data n.k.
Unaweza ukawa unajiuliza hata hivyi ni sababu gani ya msingi ambayo ilipelekea mpaka kipengele hiki kutoweka katika matoleo ya X na Zaidi.
Jibu ni dogo tuu, kumbuka mfumo wa kioo cha simu janja hizo ulianza kubadilika katika toleo la iPhone X. hapo ndipo tilianza kuona toleo la kioo ambalo kwa juu limeingia ndani kidogo.
Kupitia iPhone 8 na zile zingine za nyuma ni kwamba kulikua na nafasi kubwa kwenye kioo ambayo iliruhusu jambo hilo.
Zamani alama ya betri ilikua inaambatana sambamba na asilimia ya ujazo wa betri katika iPhone 8 na kushuka chini. Kwa sasa simu zijazo zinasubirirwa kwa hamu sana na watu wana shauku ya kutaka kujua kwamba zitakua zinaambatana na vipengele gani ambavyo viko tofauti na simu janja zingine kutoka kwa makampuni mbalimbali.
Tunajua kwamba kuna iOS mpya na simu mpya kutoka kwa Apple sio? Kupitia iOS hiyo mpya hapa ili kuona asilimia ya betri inakubidi uangalie ndani ya alama ya betri (tazama katika picha)
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je kipengele hichi ulikua unakikumbuka sana? Au hakina maana kubwa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.