fbpx

Baada ya siku na miezi kadhaa Apps za HTC zarudi Google PlayStore

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Baada ya siku kadhaa ya kuondolewa kwenye soko la apps la Google PlayStore apps za HTC zarudi na kuanza kupatikana.

Kwa kipindi cha miezi kadhaa apps mbalimbali za HTC zilianza kuondolewa kutoka soko la Google PlayStore, watumiaji wa simu za HTC au waliokuwa wanatumia apps hizo hawakuweza kupata masasisho (updates).

Apps za HTC zarudi Google PlayStore

HTC Wanahistoria ndefu katika utengenezaji wa simu za Android

Inasemekana Google walifanya mabadiliko kadhaa katika vigezo vikuu vya apps kukidhi kuwa kwenye soko hili maarufu la apps kwa simu zinazotumia Android.

Baadhi ya apps zilizoathirika ni pamoja na Sense Home, HTC Mail, RE, HTC people na zinginezo.

Baada ya timu ya utengenezaji apps ndani ya HTC kufanya maboresho yanayohitajika tayari baadhi ya apps zimeanza kuonekana katika soko hilo la apps.

INAYOHUSIANA  Study: Wape Facebook ruhusa wafuatilie utumiaji wako wa simu kisha wakulipe

Kwa sasa HTC Mail tayari imesharudishwa, na HTC wametoa uhakika hadi kufikia mwisho wa mwezi HTC Mail, RE, HTC Sense Home, HTC People, HTC Sense Companion na HTC Restore zitakuwa zimesharudi kwa watumiaji wote.

Hii ni habari nzuri kwa watumiaji wote wa simu za HTC, je ushawahi kutumia simu za HTC au kwa sasa bado unatumia? Una mtazamo gani na kampuni hii kwa sasa?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.