fbpx
Apple

Apple wamefunga maduka yake mengi nchini Marekani baada ya wizi mkubwa kufanyika

apple-wamefunga-maduka-yake-mengi-nchini-marekani
Sambaza

Apple wamefunga maduka yake mengi yanayotambulika kama Apple Store katika miji mbalimbali ya nchini Marekani ili kuepeuka wizi zaidi.

Kwa siku kadhaa sasa kuna maandamano makubwa yanaendelea katika miji mbalimbali nchini humo kupinga ubaguzi wa rangi. Maandamano haya yameendana na uvunjifu wa sheria unaohusisha ubomoaji wa maduka na wizi.

Hadi sasa tayari maduka ya Apple katika miji kadhaa – Portland, Philadephia, Brooklyn, Salt Lake City, Los Angeles, Charleston, Washington, Scottsdale na San Francisco yamekwishavamiwa na mali mbalimbali hasa hasa simu na laptop zikiibiwa.

INAYOHUSIANA  Kama Unatumia iPad Inakubidi Ufahamu Ujanja Huu!

Katika kuchukua hatua za kulinda wameamua kuanza kuyaziba maduka hayo.

Apple wamefunga maduka
Apple wamefunga maduka

Maandamano yanayoendelea nchini humo nje ya kuleta hasara kubwa kwa biashara mbalimbali – hasa hasa kipindi ambacho kuna janga la Corona lakini pia yamesababisha kuahirishwa kwa baadhi ya matukio. Sony wameahirisha utambulisho rasmi wa PlayStation 5 na pia Google wameahirisha utambulisho wa Android 11, toleo jipya la Android.

Bado hakuna dalili ya maandamano hayo kuisha hivi karibuni, na inategemewa shughuli nyingi za kiuchumi na kiteknolojia zitaendelea kuathirika.

Vyanzo: 9to5mac na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |