fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple

Apple Walipa Mamilioni Baada Ya Picha Chafu Kuvujishwa!

Apple Walipa Mamilioni Baada Ya Picha Chafu Kuvujishwa!

Spread the love

Ni Kweli Apple wamelipa mamilioni ya dola kwa binti ambae alipeleka simu yake ya iPhone ili kutengenezwa kwa wataalamu wanaofahamika na Apple.

Baada ya kuacha simu hiyo kwa ajili ya matangenezo wataalamu (mafundi) hao waliona picha hizo za huyo binti ambae ni mwanafunzi (kwa kipindi hicho).

Mafundi hao (wawili) waliamua kuchukua picha hizo na kuzipandisha katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Jambo hili ambalo lilimletea msongo wa mawazo binti hiyo na kumuharibia kabisa kiasaikolojia. Tukio hili zima limetokea mwaka 2016 ila malipo yamefanyika hivi karibuni sababu kesi ilikua inaendelea.

SOMA PIA  Simu janja bilioni 1.43 Ziliingizwa Sokoni Mwaka 2015, Rekodi Yawekwa

Kituo cha kurekebisha simu na vifaa vingine vya Apple cha huko California ambacho kinajulikana kamaa Pegatron ndicho kilichokumbwa na sekeseke hilo baada ya wafanyakazi wake wawili kufanya hivyo.

Matengenezo iPhone

Matengenezo iPhone

Kituo kimekubali na kukiri kuwa huo ni moja kati ya ukiukwaji mkubwa sana wa faragha ya wateja wake katika kituo hicho na pia ni tukio ambalo linaleta msongo wa mawazo ambao unaenda kuharibu saikolojia.

SOMA PIA  iCar; Apple yapewa ruhusa ya kufanyia majaribio magari yake yanayojiendesha yenyewe

Mwanasheria ambae alikua anaendesha kesi hiyo alifungua majadiliano ya dola milioni tano na Apple ili wasikilizane katika kutatua kesi hiyo bila kwenda mbali (kisheria) zaidi

Apple walikubali kulipa kiasi cha pesa ambacho hakipo wazi, wengi wamekua wakikiita ‘mamilioni ya dola’.

Licha ya hili Apple wamekiri kabisa kuwepo kwa kesi hiyo na wamesema wao wanachukulia swala faragha za wateja wao kwa uzito mkubwa sana.

SOMA PIA  Huawei yaizidi Apple kimauzo

Pia Apple imekubali baada ya tukio hilo kutokea wamejikita zaidi katika kuhakikisha wanatoa matamko/mafunzo na wanatilia mkazo mkubwa kwa wale wanaofanya kazi kwa niaba yao (mfano wauzaji simu na mafundi ambao wameaidhinishwa na Apple).

Ningependa kusikia kutoka kwako, nipe maono yako juu ya hili… niandikie hapo chini katika eneo la comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania