fbpx

Apple waamua kuweka kando AirPower

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Imekuwa kama desturi ya makampuni mengi wakati wa uzinduzi wa bidhaa fulani basi kuna vitu vingine pia vitawekwa wazi siku hiyo mbali na vile ambavyo vimekuwa vikiongelewa sana kabla ya uzinduzi wake. Mwaka 2017, Apple walizindua iPhone X pamoja na AirPower lakini tangu wakati huo haikuingizwa sokoni.

Sisi wateja wa bidhaa za kidijitali furaha yetu ni kuweza kuchaji vitu vingi kwa wakati mmoja na divyo ambavyo Apple walikuwa wamefikiria kuweza kuwawezesha nawaomiliki bidhaa za kampuni hiyo kufurahia teknolojia ya aina yake. Unafahamu AirPower ni nini? AirPower ni kifaa ambacho kinaweza kuchaji bidhaa kama iPhone, Apple Watch na AirPods kwa wakati mmoja na sehemu moja.

kuweka kando

AirPower: Bidhaa ambayo Apple wameamua kuweka kando ingawa ilitambulishwa pamoja na iPhone X mwaka 2017.

Sasa basi kama umekuwa mfuatiliaji mzuri na ulikuwa ukisubiri AirPower kuiniga sokoni ondoa mategemeo ya kuiona bidhaa hiyo na hii inatokana na taarifa rasmi kutoka kwa wahusika kuhusu kuachana na bidhaa hiyo kutokana na kwamba kutofikia matarajio yao iwapo ikiingia sokoni; taarifa hiyo inakuja bada ya mwaka mmoja na nusu kuchelewa kuinigzwa sokoni.

kuweka kando

Maneno ya Makamu wa Rais anayesimamia utengezaji wa vipuri kwa bidhaa za Apple yakieleza kuhusu kuweka kando AirPower ingwawa wanaamini katika teknolojia ya kutotumia waya.

Hivyo ndivyo mambo yalivyo na hii inamaanisha kuwa sio kila kitu ambacho kinatambulishwa siku ya uzinduzi basi kitaletwa sokoni. Hii inaweza kuwa ni huzuni kwa walikuwa wanategemea AirPower lakini pengine kuna kitu kingine kizuri zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Tigo na Halotel inakua kwa kasi, Airtel na Vodacom wanapoteza.. ????#Ushindani
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.