Kama kawaida yao Apple ni kampuni ambalo lipo mstari wa mbele katika kubuni vitu mbali mbali ambavyo kwa namna moja au nyingine vitamfanya mteja wao anaendelee kubaki kwao.
Taarifa zilizopo ni kwamba kwa sasa kampuni hiyo iko mbioni kufanya majaribio ya teknolojia ya 5G huko nchini marekani.
Teknolojia ya 5G itakuwa ni ya kisasa zaidi ukilinganisha na hii inayosumbua kwa sasa (4G LTE). Kwa tanzania nimebahatika kutumia teknolojia ya 4G LTE za makampuni mengi kama vile kutoka katika kampuni ya simu ijulikanayo kama Smart ambalo lina vivurushi ya bei rahisi kabisa
Kwa teknolojia hii ni wazi kabisa kuwa kampuni ya Apple inayo dhamira ya kuimajiimarisha zaidi katika swala zima la kuunganisha na mtandao (connectivity)
Majaribio hayo yatafanyika katika maeneo mawaili nchini marekani na baada ya hapo kulingana na majibu yatakayopatika ndipo tutapojua mengi kuhusiana na teknolojia hii
Lakini bado kumbuka Apple sio kampuni pekee ambalo linajikita katika kuja na teknolojia yenye kasi zaidi kuachana na 4G LTE. Kuna makampuni mengi ambayo yanafanya juu chini kuhakikisha kuwa yanaleta mapinduzi hayo.
Hii imekaa poa sana kwa kampuni ya Apple kwani itawaongezea sifa nyingi sana juu ya vifaa vyao.