fbpx

Apple kufanya uzinduzi wa tofauti sana Machi 27

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Tayari mialiko imeshatunwa kwa watu mbalimbali ili kuja kuhudhuria uzinduzi ambao unatarajiwa kuwa wa kipekee sana kutokana na sehemu utakapofanyikia uzinduzi huo na hata soko la bidhaa zenyewe.

Apple ambao wanajulikana kwa kufanya uzinduzi katika kumbi mbalimbali na hata kudiriki kujenga ukumbi wao wenyewe kwa ajili ya shughuli mbalimbali lakini Machi 27 mwaka huu (2018) wanatarajia kuzindua bidhaa zao kitofauti.

Je, uzinduzi huo utakuwa wa kitofauti kivipi?

Apple watafanya uzinduzi huo katika shule moja ya sekondari iliyopo Chicago, Marekani na sababu ya kuamua kufanya uzinduzi kwenye shule ya sekondari ni dhima ya tukio zima; uzinduzi wa bidhaa zinatazolenga sekta ya elimu na kuonyesha teknolojia mpya zinaweza kutumiwa na walimu pamoja na wanafunzi.

INAYOHUSIANA  Jinsi Gani Ya Kutumia Mfumo wa BitTorrent!

Mara ya mwisho Apple kufanya uzinduzi kwenye shule ya sekondari ilikuwa mwaka 2012 jijini New York.

CEO wa Apple, Bw. Tim Cook akiwa na watoto wa shule alipohimiza somo la uandishi wa programu (coding) kufundishwa mashuleni.

Vinavyotarajiwa kuzinduliwa Machi 27.

Mbali na kuwa Apple watazindua vifaa vya kiteknolojia vitakavyolenga sekta ya elimu zaidi mathalani iPad ya inchi 9.7 mahususi kwa ajili ya elimu itakayokuwa inauzwa $259 na kutokuwa na teknolojia ya FaceID; iPad zitakazokuwa na teknolojia ya hali ya juu ya kamera, Animoji na ARKit zinatarajiwa kutoka baadae mwaka huu.

INAYOHUSIANA  Skype - Wakuwezesha Kuchati na Kuzungumza na Watu Mbalimbali KTK Lugha Zao Bila Wewe Kuzifahamu!

Inasemekana katika uzinduzi huo wanatarajia kutambulisha toleo jipya la MacBoook Air ambayo ni miaka sasa imepita bila toleo jipya la kompyuta hiyo kutoka; hata bei yake inaweza kuwa kati ya $799-$899|zaidi ya Tsh. 1.8M-2,025M ili kuwezesha watoto wa sekondari na vijana walio vyuoni kuweza kununua.

Huwenda katika uzinduzi huo Apple wakatoa masasisho ya kalamu mahususi zitakazotumika kwenye iPad.

Kubwa zaidi Apple wanatarajiwa kutumia teknolojia ya AR (Augmented Reality) kuwapeleka watoto kwenye safari kujionea mapya waliyoyaleta kwenye ulimwengu wa elimu ikiambatana na matumizi ya teknolojia kuwaelimisha wanafunzi mashuleni.

Vyanzo: Gadgets 360, ARS Technica

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|