fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Air Tag Android Apple apps Intaneti simu Teknolojia Uchambuzi

Apple imetoa programu ya Android kwaajili ya kutafutia AirTag

Apple imetoa programu ya Android kwaajili ya kutafutia AirTag
Spread the love

Watumiaji wa Apple walianza kutumia na kupata vifuatiliaji vya AirTag kwa zaidi ya nusu mwaka na sasa watumiaji wa Android pia wanaweza kuvitumia. Kampuni ya Apple imetoa programu ya Android ambayo inaruhusu wale walio na programu endeshi hiyo kupata AirTags.

Programu, inayoitwa Tracker Detect itaruhusu watumiaji wa Android kutumia mtandao wa Apple wa “Find my Network” ili kupata AirTags na vifuatiliaji vingine. Apple imekuwa na programu hii ya utambuzi inayofanya kazi kwa muda mrefu sasa na itawatahadharisha watumiaji mara moja ikiwa na wakati wanafuatiliwa kupitia AirTag au kifaa kingine kama hicho.

SOMA PIA  Black Friday ni nini? - Siku Yenye Punguzo Kubwa la Mauzo Mtandaoni

Wale wanaovutiwa na programu watahitaji kuhakikisha kuwa kifaa chao kinatumia angalau Android 9 ili kuipakua na kuitumia. Itachukua sehemu ndogo kwenye simu yako MB19, kwa hivyo hutahitaji kuwa na wasiwasi kuhusu nafasi itakayobaki kwenye simu janja yako.

Apple imetoa programu

Picha: Muonekano wa AirTag

Kulingana na maelezo ya programu kwenye Google Play, “utaweza kutafuta vifuatiliaji vya bidhaa ambavyo vimetenganishwa na mmiliki wao na vinavyoendana na mtandao wa “Apple’s Find My”. Vifuatiliaji hivi vya bidhaa ni pamoja na AirTag na vifaa vinavyotumika kutoka kwa makampuni mengine. Ikiwa unafikiri kuna mtu anatumia AirTag au kifaa kingine kukufuatilia, unaweza kuscan na kukitafuta kilipo.

SOMA PIA  Ufahamu undani wa simu janja Samsung Galaxy M32

Chanzo: ReviewGeek na vyanzo vingine.

Endelea kutembeea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania