Hii ndio bidhaa ya kwanza kabisa ambayo inatambulishwa na kampuni ya Apple kwa mwaka 2023 na hizi si zingine ni MacBook Pro mbili zinazotumia chip za M2
Chip hizo za M2 na zenyewe ziko mbili (kumbuka hata MackBook Pro zimekuja katika aina mbili) hivyo basi kutakua na chip za M2 Pro na M2 Max.
Hapa kwa haraka haraka ni kwamba chip ya M2 Pro inakuja na CPU yenye uwezo wa Cores mpaka 12 wakati chip ya M2 Max inakuja mpaka na Cores 38 katika GPU.
Ni wazi kwamba chip hizi zote mbele zipo dhahiri katika kusaidia utiririkaji mzuri wa kazi wakati wataalam (kama vile waandaji wa mdungo, wachoraji, mainjinia n.k) wakiwa wanafanya kazi kupitia katika kompyuta hizi.
Kingine ni kwamba MacBook zinazotumia chip hizi zitakua na ubora na uharaka wa zaidi ya 40% ukilinganisha na zile za nyuma yake.
Chip hizi zinapatikana katika MacBook Pro za ichi 14 na 16 na vile vile hata katika kompyuta za Mac Mini.
Taarifa hizi zimetangazwa na Apple wenyewe tarehe 17 baada ya fununu nyingi kusambaa kama Apple wangetambulisha bishaa hizo kupitia katika jukwaa lake linalojulikana kama NewsRoom.
Ukiachana na chip hizo kuwa za aina yake bado kompyuta hizo zinakuja na sifa kadha wa kadha kama vile uboreshwaji katika teknolojia ya WiFi, uwezo mkubwa wa kukaa na chaji wa mpaka masaa 22, 8K HDMI na mengine mengi.
Ningependa kusikia kutoka kwako, hebu niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unaweza ukaanza kutumia matoleo haya mapya na kuachana kabisa na ya zamani kwa sababu ya chip?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.