Kampuni ya Beats ambayo iko chini ya kampuni ya Apple iko mbioni kuja na ‘ear buds’ ambazo zitakwenda kwa jina la Beats Studio Buds. Taarifa zilizopo ni kwamba tutarajie matoleo mawili.
Matoleo hayo yanaenda kwa majina ya A2512 na A2513. Apple ukiachana na kufanya vizuri kwa Airpods zao ambazo ni maarufu sana, wameona ni vyema kujiendeleza zaidi katika teknolojia ya vifaa vya simu.
Beats Studio Ear buds zitakuja kwa sura ya kipekee kwani hazifanani kimuonekano na Airpods kabisa. Mpaka sasa hakuna taarifa za kiundani juu ya bidhaa hii
Tupate Picha Jongefu Kidogo…
Animations of Beats Studio Buds: 🧵 pic.twitter.com/XYVvYP7ez3
— Steve Moser (@SteveMoser) May 17, 2021
Animations of Beats Studio Buds: 🧵 pic.twitter.com/XYVvYP7ez3
— Steve Moser (@SteveMoser) May 17, 2021
Baada Ya Kupata Picha Jongefu Sasa …
Pia zitakuja na teknolojia ile ya inayojulikana kama ‘Active Noise Cancellation (ANC)’ ambayo kwa haraka haraka ni kwamba inachuja kelele za nje kutoweza kuingia ndani ya sikio wakati unakua usikiliza kitu (mfn. mziki) kupitia eear buds hizo
Beats Studio Buds zitakua zina teknolojia ya kutumika bila waya (wireless). Ni wazi kwamba Apple wanazidi kujikita katika teknolojia za nje ya simu. Hii ikiwa ni kama moja ya sehemu za kukua kupitia vifaa vya simu.
Endelea kuwa na sisi maana taarifa kamili juu ya Beats Studio Buds ikitoka wewe ndio utakua mtu wa kwanza kujua hiyo basi usisahau kutembelea mtandao wetu na page zetu kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia!.
No Comment! Be the first one.