Tulisha andika hapa kuhusiana na mchakato mzima wa jinsi ya kupiga kura tuzo hizi za Microsoft.
Kusoma tena Makala ya nyuma kuhusiana na tuzo hizi ingia >>HAPA<<
Leo sasa tunakuletea washindi (App zilizoshinda) wa tuzo hizi
Vipengele kama tulivyosema vilikua ni vitatu, yaaani File management, Utility na Open Platform
Washindi Ni Kama Ifuatavyo
1.Kipengele Cha Utility
Katika kipengele hichi kuna washindi wawili ambao wamepata kura za juu kabisa.. mmoja ni ShareX na mwingne ni Ookla.
Ookla ni maarufu sana na kazi yake kubwa ni kujaribu spidi ya mtandao (internet) katika kompyuta
ShareX kazi yake kubwa ni kuchukua picha au kurekodi eneo fulai katika uso wa kioo cha kompyuta.
2.Kipengele Cha File Management
Hapa pia kuna washindi wawili, mshindi wa kwanza akiwa ni Files na mwingine ni Rufus.
Files kazi yake kubwa ni kufanya kazi kama vile ‘file explorer’ tuu na ni moja katika ya App za zamani kidogo na yenye msaada mkubwa tuu.
Rufus kazi yake kubwa ni uwezo wake wa ku’format USB (Bootable USB drives).
3.Kipengele Cha Open Platform
Kupitia kipengele hiki Microsoft iliruhusu watu waweza kupata washindi watatu, tofauti na vipengele vingine hapo juu
Hapa washindi ni Auto dark Mode, EarTrumpet Na ModernFlyouts
Auto Dark Mode kazi yake kubwa ni kuhakikisha inacheza na rangi mbili nyeusi na nyeupe ili kuhakikisha inakupa mwanga mzuri kulingana na mazingira (inafanya mambo hayo yenyewe)
EarTrumpet kazi yake ni kuweza kukuruhusu kuweza kucheza na sauti katika App tofauti tofauti na maeneo mengine mengi kwa kukuletea ‘menu’ inayoelea
ModernFlyouts hii kazi yake kubwa ni kukusaidia kusasisha kubadilisha muonekana wa mistari ya sauti (kushusha na kupandisha) na kukuletea ya kisasa zaidi.
Vile vile kampuni haikuishia hapo, waliweza kuweka machaguo ya app zao bora kutoka kwenye machaguo ya wahariri wao.
Kipengele hichi walikipa jina la Microsoft Store Editor’s Choice Awards
Washindi Ni Kama Ifuatavyo
- BURUDANI – Video: Disney+
- BURUDANI – Sauti Na Muziki: Spotify
- UBUNIFU – Graphics na 3D: Canva
- UBUNIFU – Sauti na Video: Wondershare Filmora
- UZALISHAJI: LiquidText
- KIJAMII: Discord
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Uwanja Wa Comment, Je Unakubaliana Na Tuzo Hizi? Zina Haki Ya Kushinda?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.