fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps

App Ya Kupima Uwezo Wa Simu Kutoingia Maji!

App Ya Kupima Uwezo Wa Simu Kutoingia Maji!

Spread the love

Kizuri kuhusu App hii ni kwamba unapima uwezo wa simu janja kutoingia maji bila ya kutumia maji. Najua hapa unaweza jiuliza kwamba inawezekanaje bila kutumia maji, lakini …….

Teknolojia inazidi kutushangaza siku hizi maana hata yale ambayo tulikua hatuyadhanii kabisa siku hizi tunayafanya tena kwa urahisi kabisa.

Water Resistance Tester App

Water Resistance Tester App

Kingine ni kwamba siku hizi simu janja nyingi zinaingia sokoni katika hali ya kwmaba tayari zinakua na uwezo mkubwa wa kuzuia kuingia maji. Ukiachana na hivyo uwezo wa kuingia maji katika simu hizi unapimwa na kina.

Hapa cha msingi ni kwamba App hii inawasaidia watu kujua uwezo wa simu zao kuzuia kuingia na maji bila kuingiza katika maji… kwa kiasi kikubwa jambo hili linasaidia mtumiaji kuweza kujiamini zaidi na jambo hili.

App hii inapatakana kwa android (Play store)  –> Hapa <–

SOMA PIA  Google Calendar yaongezewa vipengele vizuri sana

Hapa kinachofnayika ni kwamba sensa inasoma presha iliyoko ndani ya simu na kisha App inafanya kila kitu katika kuhakikisha kwamba inakupa majibu ya kutosha kuhusiana na simu janja yako na uwezo wake wa kuigia maji.

Angalia video hii fupi ikiwa kama ni mfano wa kupima uwezo wa simu

SOMA PIA  Google Podcast na downloads milioni 100, App ya Podcast ya Google yapaa kwa watumiaji

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umeipokeaje? je ni App nzuri au kwa sasa haina maana maana simu nyingi zinakuja na uwezo huo.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania