Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Android, Apple, apps

App Inayokuwezesha KuScan Picha Kutumia Simu-Janja!

app-inayokuwezesha-kuscan-picha-kutumia-simu-janja

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Albamu zetu za kuwekea picha haziwezi kusahaulika kwa kua kuna picha zetu za nyakati tofauti tofauti tuzipendazo.Kila kitu siku hizi ni digitali, albumu zetu zipo ndani  na picha za zamani tuzipendazo. Hebu fikiria vipi kama tunaweza kuzifanya picha hizo kuwa kidigitali kabisa (kama vile ndani ya simu)?

Tuna deni la kuzifanya picha zetu kuwa kidigitali. Kwa nini hatufanyi hivyo sasa?, kwa sababu ni wavivu, ndio. lakini hata hivyo ni kwa sababu ni kazi kubwa kidogo. Ni vigumu sana kuona mtu anapoteza mda wake na ku ‘scan’ picha zake za zamani ili azipate katika mfumo wa kidigitali, hata hao watumiaji wa ‘scanner’ ni wachache sababu wengi sio watumiaji. Wengine huwa wanapiga picha, picha zao za karatasi na simu zao (ha!). Scanner nyingi hazifanyi kazi 100% hata uki ‘scan’ picha bado itabidi ufanye marekebisho mengine ili itokee vizuri zaidi. Kitu ambacho kilibidi kiwe chepesi na cha kutumia mda mchache kinaweza kukupotezea mda.heirloom-hero

INAYOHUSIANA  Kuwa Makini App Za Bure Zinaweza Kuiba Data Zako!

Sasa App mpya inayoitwa “Heirloom” inasaidia badilisha yote hayo. Dhana yake ni rahisi sana: App inatumia kamera ya simu kama “DIY scanner” hii inaweza onekana kama ni njia mbaya na ya hadhi ya chini (mbaya), lakini Heirloom ina njia za mbinu ya kuzifanya picha hizo ziwe poa zaidi .

Cha kwanza App yenyewe ina uwezo wa kugundua mipaka ya nje na ndani ya picha, ku ‘crop’ ili kupunguza mazingira ya nyuma na kufidia sehemu zilizovurugwa na pembe (angle) picha ilivyopigwa. Pia  App ina ‘Filters’ (unajua, kuzifanya zile picha za rangi kuwa na rangi nzuri zaidi) na kuzi ‘Share’ katika mitandao maarufu ya kijamii

INAYOHUSIANA  Watumiaji WhatsApp, Facebook, Instagram kuwezeshwa kutumiana ujumbe

Heirloom-app-iOS_Moments

Hakuna haja ya kusubiri ‘scanner’ ifanye kazi yake ya ku ‘scan’, pia haina haja ya kuweka picha zako katika sehemu maalumu yaani cha kufanya ni kuzipiga picha zizo picha zako kwenye simu na kisha kuzifanyia makeke (mbwembwe) katika App hii ya “Heirloom” na kisha kuzituma katika mitandao ya kijamii.

Kote katika  iOS na Android App hii inaweza ikashushwa (tena buree!), hata hivyo unatakiwa kuwa na simu yenye kamera ya uwezo mkubwa, fikiria labda yenye ‘mega pixel’ 8 na kuendelea. Tembelea kurasa zetu za Twitter, Facebook na Instagram upate makala za kijanja.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*