Hii ni mahususi kwa wale wenye ulemavu japokua hata mtu ambae hana ulemavu ana uwezo wa kutumia kipengele hichi. Ni wazi Android imefanya jambo jemba sana kuna na sasisho hii.
Vipengele hivi vilivyoongezwa vinaitwa ‘Camera Switches’ na ‘Project Activate’ vyote hivi viwili vitakua na kazi tofauti lakini vyote vitakua vinatumika kwa kutumia uso wa mtumiaji
Kapokua wengi wanasema kwamba vipengele hivi ni mahususi kwa wale wenye ulemavu ni kwamba hata mtu ambae ni mzima kabisa anaweza akatumia vipengele hivi.
Camera Switches
kipengele hichi ndani yake kuna vitu sita ambavyo ni — angalia kulia, angalia kushoto, angalia juu, tabasamu, pandisha nyusi juu na fungua mdomo —
Hii inamaana kwamba kwa kutumia sehemu hizo (katika uso) tajwa hapo juu unaweza tumia simu yako kwa kwenda au kusogea sehemu mbali mbali.
Uzuri mwinigine ni kwamba unaweza hata kufungua eneo la ‘Notification’ kurudi katika uso wa nyumbani (home) na vingine kwa kutumia ishara hizo.
Ili kutumia kipengele hichi (camera switches) ingia katika eneo la settings na kisha nenda katika accessibility kama ukikikosa basi ingia katika soko la playstore na kisha shusha —> Hapa <—
Baada ya hapo ingia katika Switch Access na kisha unaweza anza kuweka ishara na kazi zake unazotaka ziwe zinafanyika katika simu janja yako.
Project Activate
Hiki ni kipengele kingine kabisa ambacho Android imekuja nacho na hichi kazi yake kubwa pia ni kusaidia watu kuweza kwenda katika maeneo mbali mbali ya simu janja zao kwa kutumia ishara za uso.
Kutumia alama zile zile za uso (nilizotaja katika camera switches) unaweza weka isha na ikawa ni kama kusema msemo, kutuma meseji au hata kupiga simu
Mfano mzuri juu ya kipengele hiki ni kwamba mtu anaweza kujibu kwa uharaka ya maswali ya ndio na hapana.
Japokua kwa kiasi kikubwa kwa sasa kuna maeneo mengi ambayo bado hayajapata kipengele hichi lakini maeneo machache kama vile Marekani, Ulaya, Canada na Australia wanaweza pata huduma hii huku sehemu zingine zikiwa zinaongezwa.
Kipengele hichi kinapatikana kwa kuingia na kukishusha katika soko la app la Playstore, Ingia —> Hapa <—
Ningependa kusika kutoka kwako, Hili kutoka android unalipokeaje? niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Temebelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwa Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.